Friday, 20 September 2013

Wito: Hali ya nyumba za walimu wa shule alikosomea Mwl. J.K. Nyerere

 Picture
Picha ya moja ya nyumba za walimu wa shule ya msingi Mwisenge. (picha Bundala W/KB blog)
Na Bundala William via blog — Hapa ndipo aliposoma hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na hii ndiyo hali halisi ya nyumba za walimu zilivyo sasa.

Tutafakari na kujiuliza kwa pamoja kama tutaendelea kuisubiri serikali izikarabati au tutachukua jukumu sie wenyewe. Serikali imejitahidi sana kwa upande wa madarasa kwani kwa kiasi madarasa ya shule hii ni ya kisasa na yanaridhisha. Lakini 
tunapozitazama nyumba za walimu wa shule hii, inatia huruma sana. Nyumba ni za matope na za muda mrefu sana. Zimechakaa.

Hakuna sababu tena ya  kuisubiri serikali.  Ni lazima kamati ya shule ibuni mbinu mbadala ya kuisaidia shule yao. Pia kuna viongozi wengi sana nchi hii wamesoma katika shule hii na wana nyadhifa mbalimbali, je wanafikiria shule hii?

Ni jukumu letu, marafiki wa elimu, wanajamii, wazazi na kamati za shule kuhakikisha tunafanikisha ujenzi wa nyumba za walimu wa shule ya msingi Mwisenge na zote za wilaya ya Musoma Mjini.

Marafiki wa elimu tunaanza kampeni sasa.

Ikiwa umeguswa na taarifa hii tafadhali wasiliana na marafiki wa elimu musoma kwa e-mail jmrchrd@yahoo.com  na tutakuunganisha na Kamati ya Shule ya msingi Mwisenge ili kwa pamoja tujitolee kusaidia shule hii iliyo mfano kwa Taifa.