Tuesday 8 October 2013

Bunge la Rwanda laanza kazi


Rais Paul Kagame 

Posted  Jumatatu,Oktoba7  2013  saa 16:47 PM
Kwa ufupi
Bunge hilo linatarajiwa kupitia ripoti mbalimbali za kamati za kisekta na kuzithibitisha.

Kigali. Spika mpya wa Bunge la Rwanda, Donatille Mukabalisa ameanza kuzimamia vikao vya Bunge baada ya kuapishwa rasmi Ijumaa iliyopita.
Katika vikao hivyo vilivyoanza leo Jumatatu, moja ya majukumu muhimu kwa wabunge hao ni kupitia na kuthibitisha agenda muhimu za kusimamiwa na Bunge hilo.
Bunge hilo lilichaguliwa kupitia uchaguzi mkuu wa Bunge uliofanyika Agosti mwaka huu na kutoa wingi wa viti kwa chama tawala cha RPF chini ya Rais Paul Kagame.
Wabunge hao wamepewa jukumu la kupitia na kuharakisha miswada muhimu iliyokuwa imewekwa kiporo na masuala muhimu yanayotakiwa kupewa kipaumbele ili kuharakishwa na Serikali.
Mkuu wa Mawasiliano wa Bunge hilo, Augustin Habimana amesema kwamba yapo mambo mengi yanayotarajiwa kupitiwa na Bunge hilo ikiwemo kupanga ratiba ya kujadiliwa kwa miswada hiyo na kupitishwa.
Pia Bunge hilo linatarajiwa kupitia ripoti mbalimbali za kamati za kisekta na kuzithibitisha.
 Bunge linao wajibu wa kupokea, kujadili na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kupitishwa kwa miswada 13 iliyoshindwa kupitishwa kwenye Bunge lililopita.

SOURCE: MWANANCHI