Na Lilian Lucas
Posted Jumanne,Oktoba15 2013 saa 24:0 AM
Posted Jumanne,Oktoba15 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Akizindua wa mradi huo, Kamanda wa Polisi Morogoro,
Faustine Shilogile alisema mradi huo ni moja kati ya programu nyingi
zilizoanzishwa na jeshi mwaka 2006 kwa lengo kuboresha utendaji kazi wa
polisi.
Morogoro. Jeshi la Polisi Morogoro limezindua
mradi wa kikosi kazi chenye askari wasiopungua 15 kwa kila tarafa ambao
watakuwa na majukumu mbalimbali ikiwemo ya kufuatilia na kutambua
wahalifu sugu.
Akizindua wa mradi huo, Kamanda wa Polisi
Morogoro, Faustine Shilogile alisema mradi huo ni moja kati ya programu
nyingi zilizoanzishwa na jeshi mwaka 2006 kwa lengo kuboresha utendaji
kazi wa polisi.
Shilogile alisema kila tarafa itakuwa na askari wa kikosi kazi hicho wasiopungua 15.
“Kazi yao kubwa itakuwa kutambua makosa
yanayofanyika, makundi yanayofanya uhalifu, kutatua kero zote
zinazohusiana na masula ya kuihalifu, kuwashirikisha wadau kushiriki
masuala ya ulinzi na usalama katika jamii,” alifafanua zaidi Kamanda
Shilogile.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI