Rais Kikwete akizungumza leo mkoani Pwani, amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini Tanzania, kuhakikisha shule zote za sekondari za kata, zahanati zote na vituo vya afya kwenye kata zote nchini kuwekewa umeme haraka iwezekanavyo.

Ameagiza kuwa katika maeneo yote yanayopitiwa na umeme wa gridi ya taifa, shule hizo na maeneo yaliyotajwa yapatiwe umeme wa gridi haraka na maeneo ambako hakuna umeme wa gridi, basi umeme wa solar ukafungwe kwenye maeneo hayo.

Hili ni agizo la Rais na limetakiwa kutekelezwa mara moja na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini