Tuesday, 8 October 2013

Marekani yaiasa Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame, akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni, .Marekani imeitaka Serikali ya Rwanda kutoa ushirikiano utakaosaidia kuacha  mapigano  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.PICHA | MAKTABA 

Posted  Jumanne,Oktoba8  2013  saa 13:28 PM
Kwa ufupi
Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power alisema kuwa, Rwanda ikiwa ni nchi jirani na Kongo inapaswa kuwa na nafasi ya moja kwa moja katika mchakato wa kuleta amani na utulivu nchini Kongo.

Washington.Marekani imeitaka Serikali ya Rwanda kutoa ushirikiano utakaosaidia kuacha  mapigano  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power alisema kuwa, Rwanda ikiwa ni nchi jirani na Kongo inapaswa kuwa na nafasi ya moja kwa moja katika mchakato wa kuleta amani na utulivu nchini Kongo.
Power alisisitiza kwamba nchi zote za eneo la Maziwa Makuu ya Afrika zinapaswa kufanya juhudi maradufu za kuwatokomeza waasi walioko mashariki mwa nchi hiyo.
Juzi  ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliyataka makundi ya waasi mashariki mwa Kongo kuacha kuendeleza machafuko katika eneo hilo.
Serikali ya Jamhuri ya Kongo imeshakaa na wapiganaji wa kundi la M23 mara kadhaa lakini mpaka sasa bado hakuna makaubaliano kamili baina yao.

SOURCE: MWANANCHI