Uthibitisho huu umetoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Brof Rwekaza Mukandala kuwa Katibu Mtendaji wa NECTA Dr Joyce Ndalichako ameondoka NECTA na nafasi yake sasa inakaimiwa na Dr Charles Msonde aliyekuwa msaidizi wake.
Kwa mujibu wa Profesa Mukandala, ni kwamba Dr Ndalichako ameanza likizo ya utafiti (Sabbatical leave) ya mwaka mmoja kuanzia Oktoba mosi mwaka huu hadi Septemba 30 mwaka 2014 licha ya kuwepo kwa taarifa za kuwepo shinikizo la kisiasa lilikuwa likimzonga Dr Ndalichako kutakiwa kujiuzulu.
SOURCE: JAMII FORUM
HABARI ZAIDI ZITAKUJA!