Saturday 14 September 2013

AU yailima barua ICC kuhusu Ruto, Uhuru


Posted  Septemba14  2013  saa 9:33 M
Kwa ufupi
Nairobi. Muungano wa Afrika (AU) umeiandikia barua Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)kuitaka kusitisha kesi za watuhumiwa wa machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 nchini Kenya.


Wataka wawili hao wafutiwe mashtaka yanayowakabili kwenye mahakama hiyo, ili kuweka uthabiti kwenye utawala wao
Nairobi. Muungano wa Afrika (AU) umeiandikia barua Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)kuitaka kusitisha kesi za watuhumiwa wa machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 nchini Kenya.
Watuhumiwa hao ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, na makamu wake William Ruto, pamoja na mwandishi Joshua Arap Sang.
Katika barua hiyo Muungano huo uliitaka mahakama hiyo kusitisha kesi hiyo mpaka ombi la kutaka kesi hizo kurejeshwa Kenya litakapoamuliwa.
AU pia inataka Ruto na Rais Kenyatta kuruhusiwa kuchagua vikao wanavyotaka kuhudhuria wakati wa kusikilizwa kwa kesi zao kutokana na majukumu yao ya kikatiba.
Kwenye barua iliyoandikwa kwa ICC, AU ilisema kuwa mahakama hiyo mwanzo ilipaswa kuamua kuhamishia kesi hizo nchini Kenya kabla ya hata kuanza kuzisikiliza.
Katika barua hiyo ilidaiwa AU pia iligusia suala la rufaa ambayo iliwasilishwa katika mahakama hiyo na mwendesha mkuu wa mashtaka Fatou Bensouda dhidi ya kumruhusu Ruto kuhudhuria tu baadhi ya vikao.
Muungano huo ulielezea kuhusu mikutano mikuu miwili ya usalama inayotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu ambayo Rais Kenyatta hataweza kuhudhuria kwa sababu kesi ya Ruto itakuwa inasikilizwa ICC.
AU iliongeza kuwa kesi hizo zitahujumu jukumu la Kenya katika ukumbi wa kimataifa ikisisitiza kuwa hazipaswi kuathiri majukumu ya viongozi hao wawili.
AU ilisema kuwa licha ya kuwa Kenya imekuwa ikiheshimu mahakama hiyo, inapaswa kufanya hivyo kwa kuzingatia Katiba yake.
Hatua hiyo ya AU ni mwendelezo wa juhudi za wakuu wa nchi wanachama ambao walipitisha azimio la kuwalinda viongozi walioko madarakani dhini ya ICC.
SOURCE: MWANANCHI