Babu mmoja kutoka nchini Brazil mwenye umri wa miaka 74, Aparecido Castaldo, ameamua kuuacha ukapera na kumuoa mbuzi wake anayeitwa Carmelita. (wote wawili pichani)
Harusi imepangwa kufanyika tarehe 13 Octoba mwaka huu katika kanisa linaloitwa “Devil’s Church” katika mji wa Jundiai, Brazil.
Babu huyo amewahi kuoa(binadamu) mara kadhaa na ana watoto nane
Moja wapo ya sababu alizotoa kutaka kumuoa mbuzi huyo ni kwamba “hapigi domo(haongei), haombi hela za kwenda shopping, na hawezi kupata mimba”
Mbuzi huyo, Carmelita, amekula gauni yake ya harusi, tendo lililopelekea bwana harusi kumnunulia gauni lingine.
SOURCE: WATEMI