Wednesday, 11 September 2013

HELSB yafafanua utoaji mikopo elimu ya juu



Na Mwandishi Wetu

Posted  Jumatano,Septemba11  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Tuna bajeti ya Sh306 mil kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi 99,000 kwa mwaka huu na ni wale waliotimiza taratibu


Dar es Saalam. Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imesema kuwa si wanafunzi wote watakaopata mikopo kutokana na ufinyu wa bajeti iliyo pewa bodi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu Kitengo cha Mawasiliano wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa alisema mpango wa kukamilisha taratibu za ugawaji mikopo utakamilika mpaka pale Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) itakapotoa majina kamili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo mwaka ujao wa masomo.
“Tuna bajeti ya Sh306 mil kwa ajili ya kuwakopesha wanafunzi 99,000 kwa mwaka huu na ni wale waliotimiza taratibu,” alisema Mwaisobwa.
Wakati huo huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa ametoa wito kwa walionufaika na wanaoendelea kunufaika na mikopo ya elimu ya juu, kuwa tayari kulipa mikopo hiyo mara wanapohitmu masomo yao.
Kwa mujibu ya hotuba ya Dk Kawambwa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari, waziri huyo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika mahafali ya Nne ya Chuo cha Mt. Joseph Songea yaliyofanyika hivi karibu. Aliwataka wanafunzi walionufaika na wanaoendelea kunufaika na mikopo kuwa tayari kulipa mikopo hiyo mara wanapohitmu masomo yao.

source: Mwananchi