Wednesday, 18 September 2013

Magesa Mulongo:waliohusika na vurugu za Arusha wamekamatwa


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo
 Kamati ya ulinzi na usalama ya  Mkoa  wa  Arusha  inatarajia  kutoa  taarifa  ya  matokeo ya  uchunguzi  unaoendelea  dhidi ya  watu  waliohusika  na  matukio ya mabomu  yaliyoukumba  mkoa  huo  mwezi Mei na  June   mwaka  huu   na  hatua  zilizochululiwa  kwa waliohusika
Akizungumza  katika  kikao  cha  wadau  wa  uwekezaji   mkoani   Arusha  waliokutana kujadili   fursa   na  mazingira  ya  uwekezaji mkoani  humo  mwenyekiti wa kamati hiyo  ambaye  pia ni mkuu wa  mkoa  wa  Arusha Bw  Magesa  Mulongo   amesema  wote waliofanya uhalifu mkoani  humo wamekamatwa  na  taarifa  kamili  itatolewa  baadaye.
Wakizungumzia  hali  halisi ilivyo  katika  mkoa  wa  Arusha  baadhi ya  wadau wamesema  kwa sasa  hali ya  amani  inaridhisha  na  inavutia uwekezaji  kinachotakiwa  ni  kuboresha zaidi   mazingira  hayo  na  kudumisha  amani .

SOURCE: ITV-DAIMA