Tuesday, 17 September 2013

Mgeja amfagilia Edward Lowassa

Na Suzy Butondo

Posted  Jumanne,Septemba17  2013  saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Mgeja aliyasema hayo juzi wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa la African Inland (AIC) Wilayani Kahama ambayo ilisimamiwa na Edward Lowassa.

Kahama. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja amesema kuwa wale wanasiasa wenye chuki wanaomwonea wivuWaziri Mkuu aliyejiuzulu wa awamu ya nne, Edward Lowassa katika kuchangishaharambee wanahangaika na kivuli chake.
Mgeja aliyasema hayo juzi wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa la African Inland (AIC) Wilayani Kahama ambayo ilisimamiwa na Edward Lowassa.
Alisema kwa sasa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakimfuata Lowassa kwa lengo la kubeza harambee anazochangia katika makanisa mbalimbali na kuongeza kuwa kiongozi huyo kwa sasa ni kama mti wa matunda ambao haukosi kurushiwa mawe.

SOURCE: MWANANCHI