Akizungumza
na ITV wakati wa utambulisho wa mtambo huo uliofanyika hospitalini hapo
jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji Dk.Marina Njelekela amesema
mtambo huo utaanza kufanya kazi rasmi mapema mwezi ujao na kubaini kuwa
serikali itaokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa wagonjwa waliokuwa wanaenda
kutibiwa nje na nchi na kutoa wito kwa kampuni zote za bima ya afya
nchini kuwalipia wateja wao wanaohitaji huduma mbalimbali za moyo
kutokana na gharama zake kuwa juu.
Naye
mkuu wa idara ya magonjwa ya upasuaji wa moyo na utabibu hospitali ya
muhimbili Dkt.Robert Mvungi amesema pamoja na upatikanaji wa mtambo huo
bado hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
upungufu wa wataalamu ambapo amebaini kuwepo kwa madaktari 121 tu kati
ya 365 wanaohitajika.source: ITV-Daima