Thursday 12 September 2013

Taifa la Marekani na kadhia ya Septemba 11


 
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi

Posted  Alhamisi,Septemba12  2013  saa 10:4 AM
Kwa ufupi
  • Zaidi ya watu 3000 waliuawa


Taifa la Marekani jana limetimiza miaka 12 tangu Septemba 11, mwaka 2001, yalipotokea mashambulizi ya kigaidi  kwenye miji ya  New York  na Washington DC .
Mashambulizi hayo yalisababisha watu  takribani  3,000  kupoteza maisha na kuliweka taifa  hilo kwenye majonzi mazito ya kupotelewa na wapendwa  wao.
Kutokea kwa mashambulizi hayo kuliacha mshangao mkubwa kwa  Taifa la Marekani ambalo lilidhaniwa kuwa lipo imara kiusalama na  lisingeweza kushambuliwa  kwenye  ardhi yake kama ilivyotokea.
Hali ilivyokuwa
Tukio hilo lilipotokea  Jiji la New York  na Washington DC, anga lilionekana kuchafuka kwa moshi wakati ndege mbili za abiria zilizotekwa zilipogonga katika minara ya majengo ya biashara (World Trade Center ). Ndege  nyingine ziligonga  kwenye  makao makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani  Pentagon. Tukio hilo kwa ujumla lilizua mshangao mkubwa duniani kutokana na imani ya wengi kwamba Marekani ni taifa kubwa na lenye ulinzi imara.
Ndege nyingine watekaji walidhibitiwa
Katika hatua nyingine ndege ya nne iliyotekwa ilianguka karibu na mji mdogo wa Shanksville, Pennsylvania, baada ya abiria kupambana na watekaji na kuchukua udhibiti wa ndege hiyo.
Taifa hilo tajiri duniani baadaye lilibadili idara zake za ulinzi wa ndani na kubadili sheria ili kuzuia uwezekano wa mashambulizi mengine kama hayo kutokea.
Al Qaeda yahusishwa.
Tukio hilo kubwa kutokea duniani liliwahusisha wafuasi wa mtandao wa al Qaeda .
Serikali ya wakati huo ilikuwa inaongozwa na Rais mstaafu  George Bush, baada ya kutokea kwa tukio hilo  mtandao wa al Qaeda ulihusishwa na mashambulio hayo moja kwa moja.
Kumtafuta  Osama

Baada ya Serikali ya Marekani kuihusisha al Qaeda, iliamua kuivamia nchi ya Afghanistan na Iraq  na kuzishambulia nchi hizo kwa lengo la kumsaka kiongozi wa Al Qaeda  Osama Bin Laden ambaye ndiye aliyehusishwa kupanga njama za kuishambulia Marekani.
Hata hivyo tokea wakati huo ilikuwa ikijulikana kuwa Al Qaeda ni kundi lililoundwa na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA muongo mmoja kabla ya hapo wakati wa vita dhidi ya majeshi ya Urusi ya zamani nchini Afghanistan.
Viongozi wakuu wa kundi hilo hususan ukoo wa Bin Laden ulikuwa na uhusiano wa karibu wa kibiashara na baadhi ya wanasiasa nchini Marekani wakiwemo wa ukoo wa Bush.
Jambo hilo lilisababisha baada ya kutokea kwa tukio hilo Septemba 11.Mashambulizi ya maneno dhidi ya Osama Bin Laden yaliyofuatiwa na uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan.
Tangu  Marekani ilipoivamia Afghanistan,  wasomi wa Marekani walieleza bayana kuwa sera za uingiliaji wa kijeshi za Serikali zilizopita, ndizo zilizosababisha kutokea matukio ya umwagaji damu ya Septemba 11.
Kwa mtazamo wa wasomi na wanafikra hao, kama  Serikali zilizopita nchini Marekani zisingeunga mkono ukiukaji wa wazi wa misingi ya demokrasia na haki za binadamu katika pembe mbalimbali duniani na kusababisha maafa kadhaa wakati wa vita ya Ghuba ya Uajemi ya mwaka 1991, huenda magaidi wasingehangaika na Marekani.
Obama anakumbuka
Wakati Wamarekani wanakumbuka na kuadhimisha siku hiyo, Rais wa Marekani Barack Obama ametembelea  maeneo yote ambayo mashambulizi yalitokea.
Katika hotuba yake ya kila wiki alisifu watu waliofanya kazi za uokoaji ambapo  walijaribu kuokoa maisha ya wahanga wakati wa mashambulizi hayo.
Mapema mwaka huu, vikosi maalum vya Marekani vilifanikiwa kumwua kiongozi wa Al-Qaida Osama bin Laden huko Pakistan na kutimiza ahadi aliyoitoa rais wa zamani wa Marekani George W. Bush.
Hakuna hotuba
Kwa mara ya kwanza kwenye maadhimisho ya tukio hilo hakukuwepo na hotuba yoyote wakati wa sherehe hizo kutoka
Familia za zaidi ya watu waliouawa ziliruhusiwa  kufika katika eneo la tukio la mashambulizi hayo maarufu kama Ground Zero mjini New York,.
Awali idara ya afya nchini Marekani ilitangaza kuwa manusura wa mashambulio hayo na wale waliowasaidia watapewa uchunguzi na matibabu ya takriban aina hamsini za saratani bila malipo, kwa sababu walivuta hewa iliyokuwa na sumu baada ya mashambulio hayo.
Makala hii imeandikwa na, Aidan Mhando kwa msaada wa Mashirika mbalimbali ya habari
SOURCE: MWANANCHI
kwa wanasiasa.