Imebadilishwa: 11 Septemba,
2013 - Saa 13:56 GMT
Serikali ya Kenya imetangaza ugunduzi wa bwawa kubwa la maji
chini ya ardhi ambalo linaweza kumudu mahitaji ya maji katika kipindi cha zaidi
ya miaka hamsini ijayo katika jimbo la Turkana.
Bwawa hilo bila shaka litaleta afueni kwa wakaazi kwani Turkana ni eneo kame
Kaskazini Magharibi mwa Kenya.Bwawa hilo linapata maji kutoka kwa chemichemi za maji kutoka milima ya mbali kwa hivyo ikitumiwa vyema bwawa hilo huenda lisiwahi kukauka.
Mamilioni ya wakenya wanakosa maji safi.
Nchi hiyo pia inakabiliwa na msimu tata wa mvua na inakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Utafiti ulifanywa na shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO na wanasayansi wa Kenya kwa ufadhili wa serikali ya Japan.
source: BBC Swahili