Kupatikana
kwa wahamiaji haramu hao kunatokana na ushirikiano wa wananchi ambao
umesaidia kukamatwa kwa wahamiaji hao huku wakidai kuwa baadhi yao
walikosa hewa kufuatia kujificha katika mizigo hiyo
Kwa
upande wake afisa uhamiaji mkoa wa Morogoro Hamprey Minja amesema kuwa
dereva wa gari hilo amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi ambapo
amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti kwa kiasi kikubwa
maeneo ya mipaka kwa ajili ya kudhibiti matukio ya wahamiaji haramu
hali inayopelekea wahamiaji hao kutumia njia nyingine ikiwemo ya
kujificha katika magari ya mizigo
Jeshi
la polisi mkoa wa Morogoro limewaweka chini ya ulinzi wahamiaji hao
ikifanya taratibu za kuwafikisha mahakamani kujibu mashtaka ya kuingia
nchini bila kibaliSOURCE: ITV