7th October 2013
Jumamosi ya Septemba 21, mwaka huu itabaki kuwa siku
ya kukumbukwa katika historia ya Kenya, Ukanda wa Afrika ya Mashariki
na hata Afrika nzima kwa ujumla.Siku hiyo inabaki katika kumbukumbu za
waafrika wote kwa ujumla hasa kutokana na shambulio kubwa la kigaidi
lililoikumba nchi hiyo na kusababisha watu wengi kupoteza maisha yao.
Shambulio hilo lililohusishwa na Kundi la Al-Shabab na Al-Qaeda, lilitokea katika kituo cha kibiashara cha Westgate na kusababisha takribani watu 67 wasio na hatia kupoteza maisha yao. Tangu kutokea kwa shambulio hilo, tahadhari kubwa nchini Kenya imekuwa ikichukuliwa katika maeneo yote yenye mkusanyiko wa watu wengi.
Tahadhari kubwa pia inaihitajika kuzidi kuchukuliwa kwa nchi zote za Afrika Mashariki na si kwa Kenya tu, kwani makundi hayo ya kigaidi ni hatari sana hususan pale yanapodhamiria kushambulia eneo fulani.
Hata hivyo, wasiwasi wetu mkubwa ni kutochuliwa tahadhari ya kutosha na umakini zaidi katika viwanja vyetu vya soka hapa nchini tangu kutokea kwa tukio hilo la kinyama nchini Kenya. Ieleweke viwanja vya soka ni moja kati ya maeneo muhimu ambayo yanakuwa na mikusanyiko mikubwa wa watu wengi hususan pale zinapofanyika mechi zinazovuta hisia za mashabiki wengi wa soka.
Ingawa Jeshi la Polisi nchini kupitia kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba lilieleza kuwa jeshi hilo limechukua tahadhari katika kujilinda na vitendo vya kigaidi, NIPASHE bado tunaamini kama umakini upo, basi katika viwanja vya soka hakujamwilikwa ipasavyo na kunahitajika kutupiwa jicho la ziada.
Tunapatwa na wasiwasi wa kuwepo kwa umakini wa kutosha hasa baada ya shabiki mmoja wiki iliyopita kupigwa picha akiwa na bastola uwanjani hiyo ikiwa ni kinyume na sheria za Shirikisho la Soka za Kimataifa, Fifa.
Kwa mujibu wa sheria za Fifa ni kosa la jinai kwa shabiki wa soka kuingia na silaha uwanjani kama si mhusika wa vyombo vya usalama uwanjani hapo.
Shirikisho la Soka nchini (TFF), kupitia kwa Katibu wake Mkuu, Angetile Osiah limetahadharisha na kuzidi kutoa onyo likiwataka mashabiki, wapenzi wa soka na wadau wa mchezo huo kutokwenda na silaha uwanjani huku likieleza kuwa hatua kali zaidi zitachuliwa kwa watakaobainika kutenda kosa hilo.
NIPASHE tunaamini kauli hiyo itakuwa na mashiko zaidi endapo suala zima la ulinzi katika viwanja vyetu litazidi kuimarishwa, kwani kwa hali ilivyo sasa ni rahisi mtu kuingia na silaha hatari na kutekeleza azma yake.
Pamoja na utekelezaji huo, bado kuna umuhimu mkubwa wa jeshi la polisi kutoa somo zaidi kwa vyombo vyao vya usalama vinavyofanya ulinzi viwanjani hasa kutokana na namna vinavyojipanga.
Mara nyingi askari wetu wanaosimamia suala zima la usalama viwanjani, baadhi hujisahau kufanya kazi iliyowapeleka na kuwa washangiliaji wa mechi. Tunaposema semina ama darasa kwa askari wanaopangwa kusimamia shughuli nzima ya usalama viwanjani inahitajika, hii ni kutokana na vyombo vya usalama vya nchi zilizoendelea vinavyotekeleza zoezi hilo.
Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea, askari wanaohusika na usalama viwanjani, wakiwa uwanjani huwageukia mashabiki na kutazama matukio yanayoendelea jukwaani, lakini hilo ni tofauti kabisa na hapa nchini.
Katika mechi nyingi ambazo NIPASHE imehudhuria ikiwamo ya jana kati ya Yanga na Mtibwa kwenye Uwanja wa Taifa, askari wa usalama uwanjani hugeukia tu jukwaani pale ambapo kunapokuwa na kelele ambazo zinaashiria uwapo wa tukio ambalo si la kawaida. Kukua kwa teknolojia ambapo mechi huonekana karibu kila kona ya dunia, kunaweza kuzidi kutishia usalama wetu hasa kutokana na ukweli kwamba makundi ya kigaidi kama Al-Shabab na Al-Qaeda yanaweza kutumia mwanya huo kusoma udhaifu wa vyombo vyetu vya usalama viwapo viwanjani.
NIPASHE tunaamini kwamba jeshi la polisi na vyombo vyote vya usalama vitazidi kulichukulia tukio la kigaidi la Westgate nchini Kenya kama somo katika kuimarisha ulinzi kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi ikiwamo viwanjani.
Kama hilo likizembewa, basi kuna uwezekano siku moja tukajikuta tuingia katika majonzi kama ilivyokuwa Kenya, huku taifa likipoteza mapato makubwa yatokanayo na vingilio vya mechi uwanjani kutokana na watu kuhofia kwenda maeneo hayo.
Hatua hiyo pia itakuwa janga kwa klabu zetu ambazo zinajiendeshwa kwa kutegemea viingilio.
Hata hivyo, bado hatujachelewa, kwani wakati wa kujiimarisha unaweza kuanza sasa, na hili si kwa jeshi la polisi ama vyombo vya usalama pekee, bali ni jukumu la kila raia mwema kuchukua tahadhari na kutoa taarifa kwa vyombo husika pale tunapohisi jambo lolote linaloweza kuhatarisha maisha yetu.
NIPASHE tunaamini vyombo vya usalama vikishirikiana na raia wema, hakuna kitakachoshindikana katika kuchukua tahadhari dhidi ya magaidi wanaotaka kuhatarisha maisha yetu.

CHANZO:
NIPASHE