
Aliko Dangote
Kwa ufupi
Waziri wa madini wa Kenya, Najib Balala
alipongeza hatua hiyo ya Dangote na kufurahia ushirikiano wake na tume
iliyoundwa na Serikali ya Kenya ya kuchunguza utaratibu wa utoaji leseni
za kuwekeza katika sekta ya madini nchini Kenya. Balala alitumia pia
fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine katika sekta hiyo ya
Madini,ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi.
Serikali ya Kenya imewaalika wawekezaji wengine kujitokeza katika sekta ya Madini ili kukuza uchumi.
Nairobi. Miongoni mwa mabilionea
wakubwa Afrika ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa Nigeria, Aliko
Dangote amesema atawekeza dola za kimarekani milioni 400 katika sekta ya
madini nchini Kenya.
Dangote ambaye aliwasili Kenya wiki iliyopita
pamoja na Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria, alisema yuko tayari
kuwekeza katika sekta ya madini ya Kenya ili kuchangia ukuaji wa uchumi
wa nchi hiyo.
Waziri wa madini wa Kenya, Najib Balala alipongeza
hatua hiyo ya Dangote na kufurahia ushirikiano wake na tume iliyoundwa
na Serikali ya Kenya ya kuchunguza utaratibu wa utoaji leseni za
kuwekeza katika sekta ya madini nchini Kenya. Balala alitumia pia fursa
hiyo kuwakaribisha wawekezaji wengine katika sekta hiyo ya Madini,ili
kusaidia kukuza uchumi wa nchi.
“Namshukuru sana Dangote kwa kukubali kuwekeza
katika sekta hii ya madini hapa Kenya kwani atatusaidia kukuza uchumi wa
nchi yetu, pia natumia fursa hii kuwakaribisha wengine,’’ alisema
Balala.
Awali Kenya ilisema kwamba itafuata moja kwa moja
sera na mfumo wa udhibiti wa madini kama unaotumiwa na Tanzania kwa
sababu mageuzi yaliyofanywana Serikali katika sekta ya madini ni dhahiri
kuwa yameanza kuzaa matunda.
Kenya iliiwashauri Watanzania kuwa ni vyema
kupata Katiba Mpya, lakini Katiba peke yake haiwezi kuleta maendeleoya
wananchi kwani maendeleo yataletwa na juhudi za wananchi wenyewe.
Hayo yalisemwa na Balozi wa Kenya nchini, Mutinda Mutiso alipokuwa akimuaga Rais Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.
source: Mwnanachi
source: Mwnanachi