Tuesday, 10 September 2013

PICHA: AZAM TV- YAJA, SASA KUANZA NA MATANGAZO YA MPIRA WA MIGUU TU, YATUMIA VYOMBO VYA KISASA

Na. Dezidery Kajuna,
Jumanne, 10/09/2003
Tasaoblogspot.
Mmoja kati ya matajiri wakubwa Tanzania na barani Afrika, ameanza uwekezaji katika vyombo vya habari. Mara hii akianza na urushaji wa matangazo ya mpira wa miguu moja kwa moja kwa kutumia vyombo vya kisasa mithili ya vile vitumiwavyo BBC au CNN, ofisi zake zikiwa Tabata jijini Dar es Salaam.


Mfanya biashara huyo ambaye ni maarufu ndani na nje ya nchi ya Tanzania awekeza katika biashara nyingi ikiwemo utengenezaji wa vitafunwa almaarufu kama chapati, utengenezaji au uzalishaji wa unga wa mahindi na ngano, huku akiwa pia anamiliki mmoja ya timu ngeni na tajiri katika soka la Tanzania.
Huu ni mfano wa kuigwa kwa kila mpenda maendeleo. Hata hivyo, amewekeza katika bandari ya Zanzibara huku akiwa ametengeneza vizuri maenoe maarumu ya kupandia boti zake zifanyazo safari zake katika bahari ya Indi.
Azam limekuwa jina maarufu kwa sababu ya bidhaa zake lakini likiwa ni jina la kampuni yake.
Lakini je ni wangapi wanamfahamu kwa sura bila shaka ni wa chache sana. Katika makala nyingine nitawalea picha yake.
Picha na maelezo hapo chini kwa msaada wa blog ya Bin Zubeiry
IMEWEKWA SEPTEMBA 9, 2013 SAA 9:42 ALASIRIMtaalamu kutoka Afrika, Martin Botha akitoa mafunzo kwa crew ya Azam TV katika ofisi kuu za kampuni hiyo, eneo la Tabata Reli, Dar es Salaam.
Sehemu ya vifaa studio


Madishi...

Mtaalamu kutoka Marekani akitoa mafunzo kwa Jaffar Iddi kwa Crew la Azam TV

Botha akitoa mafunzo kwa Crew

Kijana wa Crew akipata mafunzo ya utumiaji wa vifaa vya kisasa

Kijana wa Crew mafunzoni katika kifaa cha kisasa kabisa

Kama CNN, au...

Mmoja wa Wakurugenzi wa Azam TV, Alhaj Yussuf Bakhresa (kulia) akiwa na Wataalamu kutoka Uingereza

Gari kubwa la kurushia matangazo ya moja kwa moja

Mtambo huo..

Gari la kurushia matangazo ya Live

Wataalamu kutoka nchi mbalimbali wakiwa kazini ofisi za Azam TV Tabata Reli

Mtaalamu kutoka Uingereza akiwa kazini

Hii maana yake Uwanja wa Taifa wapiga picha za kawaida watakuwa hawasumbuliwi- kinyonga huyu atakuwa anachukua vitu juu kwa juu..hakuna kukimbia na Kamera...

Gari dogo la matangazo ya Live

Uani

Barazani