Mvutano
huo umekuja kufuatia taarifa ya wilaya ya Kwimba iliyosomwa kwa rais
Jakaya Kikwete na mkuu wa wilaya hiyo Bw. Selemani Mzee, ambaye amesema
hali ya huduma ya maji mjini Ngudu kwa sasa ni mbaya kupindukia ambapo
idadi ya wananchi wanaopata majisafi na salama ni 11,310 tu kati ya watu
25,370, idadi ambayo ni sawa na asilimia 44.6 kutokana na mji huo
kutegemea visima virefu vitano, ambavyo vilichimbwa miaka kati ya 27 na
57 iliyopita, huku pia uwezo wa chanzo cha maji kilichopo kikiwa ni mita
za ujazo 265 kwa siku, ambapo maji hayo hutolewa kwa mgao kila baada ya
siku tatu.
Huku
kila mbunge akionekana kuvutia upande, mbunge wa Sumve Mh. Richard
Ndasa ameshauri mradi huo wa kupeleka maji katika mji wa Ngudu utokee
Magu kupitia jimboni kwake ili kuvinufaisha vijiji zaidi ya 40, huku
mbunge wa jimbo la Kwimba Mh. Shanifu Mansoor akisema kuwa ni vizuri
serikali iendelee na mpango wake wa kutumia maji ya ziwa victoria
yanayotolewa kwenye mradi wa Kahama- Shinyanga ( kashwasa ) na
kuyapeleka ngudu kutokea kijiji cha mhalo, hatua ambayo itanufaisha
vijiji zaidi ya 60 vya tarafa ya mwamashimba na Ngudu
Katika
kuweka sawa hali ya mambo, waziri wa maji Mh. Prof. Jumanne Maghembe
amesema kwamba serikali itatekeleza miradi yote miwili, ambayo ni ya
kutoa maji kijiji cha Mhalo kwenda Runere na hatimaye kufika mjini Ngudu
pamoja na ule wa kutoka wilayani Magu ambao uko kwenye mchakato wa
kumpata mhandisi mshauri wa kusanifu mradi huo, na kuongeza kuwa mradi
wa maji wa mwamashimba kwa mwaka huu umetengewa shilingi milioni 500.
Mapema
akizungumza na wananchi wa wilaya ya Kwimba wakati akifungua uwanja wa
ndani wa michezo katika chuo cha maendeleo ya michezo Malya, rais
Kikwete amesema atahakikisha miradi yote miwili inatekelezwa kama
alivyohaidi wananchi wakati wa kampeni ili kuondoa kero ya maji katika
wilaya ya kwimba yenye wakazi zaidi ya laki mbili.source: ITV-Daima