Wazazi wawili wamehukumiwa kwa kosa la mauaji ya msichana waliokuwa wamemuasili kutoka nchini Ethiopia.
Larry na Carri Williams kutoka jimbo la
Washington, walimnyima chakula na kumchapa msichana Hana Williams hadi
alipofariki katika bustani ya nyumba yao mwezi Mei mwaka 2011.Mawakili wa utetezi walikubali kuwa wazazi hao walikuwa wazazi wabaya, lakini akaitaka mahakama kujua kuwa wawili hao sio wahalifu.
Kulingana na stakabadhi kumhusu Hana, msichana huyo angekuwa na umri wa miaka 13 wakati wa kifo chake.
Wazazi hao walilaumiana wakati wa kesi hiyo kulingana na Skagit Valley Herald.
Alipatikana na hatia ya mauaji ingawa jopo la majaji halingeweza kutoa uamuzi kuhusu hukumu watakayopata wawili hao.
Wawili hao walioishi mjini Sedro-Woolley, huenda wakafungwa maisha jela.
source: BBC Swahili