Kwa ufupi
Waziri Malima aliyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo hayo yaliyoshirikisha mikoa ya Mbeya, Iringa.
Morogoro. Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Adamu Malima amewataka wahitimu wa mafunzo ya ukaguzi na
udhibiti wa mbolea, awamu ya nne kutumia mafunzo waliyoyapata ili
kukidhi matarajio ya wakulima walio kata tamaa kwa muda mrefu kutokana
na uwapo wa mbolea zisizo na viwango vya ubora.
Waziri Malima aliyasema hayo mkoani Morogoro
wakati akifungua mafunzo hayo yaliyoshirikisha mikoa ya Mbeya, Iringa,
Tabora, Siminyu, Morogoro, Mwanza na Shinyanga na kudai kuwa yatasaidia
kutatua tatizo la uchakachuaji mbolea unaofanywa na watu wasio waaminifu
na kuwataka wasimamie kwa weledi sheria ya mbolea namba 9 ya mwaka
2009.
Naibu waziri huyo wa kilimo, aliwataka wakaguzi na
wadhibiti wa ubora wa mbolea hao waliopata mafunzo hayo kurejesha imani
na matarajio ya wakulima.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI