Kamati
ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) inamsubiri mwendesha baiskeli wa
Marekani aliyepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu
mwilini, Lance Armstrong, arejeshe medali ya shaba aliyoshinda kwenye
mashindano ya Olimpiki ya mjini Sydney, mwaka 2000, amesema Mkuu wa Tume
ya Sheria ya IOC.
Kamati hiyo ilimwandikia Armstrong barua Januari, mwaka huu kumtaka
arejeshe medali hiyo, ingawa kuna taarifa kuwa mwendesha baiskeli huyo
alikiri makosa yake na kwamba kilichobaki ni kutimiza ahadi yake ya
kurudisha medali kwa IOC.
Kamati
ya Kimataifa ya Olimpiki ilichelewesha kumuadhibu Armstrong hadi
shirika linaloongoza mchezo wa mashindano ya baiskeli (International
Cycling Union-UCI) lilipoidhinisha hatua ya Armstrong kuchukuliwa hatua
baada kipindi cha wiki tatu, ambapo mtuhumiwa alikuwa na fursa ya kukata
rufaa.
Kilichofuata
ni hatua ya kumnyang’anya Armstrong medali zote saba alizoshinda kwenye
mashindano ya mbio za nchini Ufaransa, maarufu kama Tour de France na
kupigwa marufuku asishiriki tena mashindano mengine maishani mwake. Haya
yalifuatia ushahidi wa shirika la Marekani linalopambana na matumizi ya
dawa za kuongezea nguvu mwilini (USADA).
Baada
ya ubishi mkali, marafiki wa Armstrong walitoa ushahidi uliombana yeye
na baadhi ya washirika wake kuwa ni kweli alitumia dawa za kuongeza
nguvu mwilini.
SOURCE: JAMUHURI MEDIA
|