24 Septemba, 2013 - Saa 05:30 GMT
Wanasheria wanaomwakilisha Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta, wametaka mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC
kumruhusu mteja wao kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi dhidi yake
itakayoanza katika mahakama hiyo mwezi ujao.
Bwana Kenyatta anakabiliwa na kesi ya uhalifu
dhidi ya binadamu kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi yaliyoikumba
Kenya mwaka 2007.Mawakili wa bwana Kenyatta wanadai kuwa anastahili kuruhusiwa kufuatilia vikao vingine muhimu vya kusilizwa kwa kesi hiyo kupitia picha za video.
Huenda ikadhaniwa kwamba hatua ya bwana Kenyatta kutoa ombi hili wakati kumetokea shambulio la kigaidi katika jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi kuwa sadfa lakini wengi wanadhani kuwa ni mojawepo wa mbinu za kulemaza kesi dhidi yake.
Mawakili wa bwana Kenyata wametaja kwamba Naibu rais William Ruto ambaye pia anakabiliwa na mashtaka kama yake mbele ya Mahakama hiyo ya ICC ameruhusiwa hivi punde kurejea nyumbani kukabiliana na hali baada ya shambulizi hilo la Westgate mwishoni mwa juma.
SOURCE: MWANANCHI