10th October 2013
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Tanzania Bara, Philip Mangula, amesema anajuta na anaona aibu kuishi
katika Jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), na kuwataka
wanachama wa CCM kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2015 jimbo hilo linarudi
kwao.
Mangula aliyasema hayo jana alipozungumza na viongozi mbalimbali wa kata na wilaya zote za jijini Dar es Salaam pamoja na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wa CCM.
“Ni aibu mimi ni mkazi wa Oysterbay jijini Dar es Salaam, na Mdee ndiye Mbunge wangu sasa siku akisema anataka kuongea na wazee wa jimbo lake mimi ntafanyaje? siwezi kwenda nitasingizia naumwa ili nisiende,” alisema.
Alitoboa siri mbele ya wanachama hao kuwa kilichoiponza CCM mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu na kuifanya ipoteze baadhi ya majimbo na kata kutokana na kuwapo makundi, wanachama kuchukiana pamoja na kukomoana.
Aliwataka watendaji wa CCM ngazi ya kata ambao madiwani wao walibwagwa na upinzani kujitathmini ili waone kama bado wana uhalali wa kuendelea kushikilia nafasi zao.
Mangula aliwaonya wanachama wote wanaokisaliti chama kwamba adhabu yao ambayo haina msamaha ni kufukuzwa uanachama.

CHANZO:
NIPASHE