Tanzania na Zambia zimeamua kuchukua hatua za ziada kujaribu kuboresha 
usafiri kati ya nchi hizo mbili, ambazo tayari zina ushirikiano wa muda 
mrefu kupitia shirika la reli la Tazara. PICHA | FAILI 
            
Kwa ufupi
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Kodi 
Tanzania (TRA), Rished Bade, ambaye kwa jana alikuwa mkuu wa msafara, 
alisema ujumbe wake utakuwa na mazungumza na wenzao wa Zambia kwa nia ya
 kuboresha utendaji na kuimarisha uhusiano.
Mbeya. Tanzania na Zambia 
zimeanza mazungumzo maalumu ya kutafuta mbinu za kuboresha utendaji kazi
 wa kusafirisha mizigo kwenye mpaka wa nchi hizo, uliopo Tunduma.
Tayari, ujumbe wa zaidi ya watu 20 kutoka Wizara 
za Uchukuzi, Fedha, Mambo ya Ndani na wadau wa usafirishaji waliwasili 
jijini Mbeya tangu juzi, jana walikwenda Tunduma mpakani mwa Tanzania na
 Zambia kujionea utendaji ulivyo kwa upande wa Tanzania.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamalaka ya Kodi Tanzania 
(TRA), Rished Bade, ambaye kwa jana alikuwa mkuu wa msafara, alisema 
ujumbe wake utakuwa na mazungumza na wenzao wa Zambia kwa nia ya 
kuboresha utendaji na kuimarisha uhusiano.
Bade alisema baada ya ujumbe,  kitafuata kikao cha
 makatibu wakuu wa wizara zote zinazohusika za Tanzania na zile za 
Zambia kitakachofanyika Oktoba 3.
 “Pamoja na mengineyo, lengo kubwa ni kuandaa 
taratibu za kuanza ujenzi wa kituo kimoja  cha mpakani kwa magari yote 
ya Zambia  na Tanzania ( One Stop Boarder Post), ili kuondokana na 
usumbufu wa sasa,” alisema.
Alisema tayari ujumbe wa Zambia walikuwa wakijiandaa kwenye Mji wa Nakonde  nchini Zambia, kabla ya kukutana kuanzia kesho.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI