Monday, 16 September 2013

Madereva wa malori waendelea kuteseka mpakani

Madereva wa malori kutoka Tanzania wanaendelea kusota katika mpaka wa Tanzania na Rwanda baada ya ushuru wa barabara ambao uliahidiwa kushushwa na Serikali ya Rwanda, kutotekelezwa.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili mmoja wa madereva hao, Charles Sokwe, alisema eneo la Rusumo kuwa kuwa bado tatizo la ushuru limekuwa likiwasumbua.
Alisema kuwa ushuru huo umekuwa ukibadilika kama unavyokwenda kubadilisha dola kwenye maduka ya fedha.

Sokwe alisema tangu juzi yupo mpakani hapo na kwamba ilipofika majira ya saa 11 jioni walipandishiwa ushuru na kujulishwa kulipia dola 500.
Hata hivyo, Sokwe alisema kiasi hicho hakuweza kulipia hali iliyomlazimu kuendelea kuwa mpakani hapo pamoja na madereva wengine.
Alisema ilipofika jana majira ya asubuhi hadi saa 4 ushuru ulishuka na kutakiwa kulipia dola 152 baada ya muda huo kupita walijulishwa ushuru huo kupanda na kufikia dola 500.
Sokwe alisema ilipofika saa 7 mchana ushuru ulishuka na kufikia dola 152 ndipo madereva hao walipoanza kuvuka.
“Kwa sasa malori yameanza kupita baada ya kutangaza ushuru ni dola 152 ila sijajua mpaka nifikiwe hizo gharama zitakuwa zimebadilika maana hapa mpakani imekuwa kama bureu change ushuru kupanda wakati wowote,” alisema
Alisema kitendo hicho cha ushuru kubadilika kila wakati imekuwa ikiwaumiza huku wakiendelea kupoteza muda mrefu mpakani hapo.
NIPASHE Jumapili ilipowasiliana na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tzeba juu ya suala hilo alisema kuwa "Samahani nina drive na kisha kukata simu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI