Monday, 16 September 2013

Mmiliki kiwanda Moshi adaiwa kuunganisha maji kinyemela


11th September 2013
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (Ewura)
Mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha chakula cha mifugo cha mkoani Kilimanjaro, ni mmoja kati ya watuhumiwa watatu wa wizi wa maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Moshi (Muwsa).

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuisababishia Muwsa  hasara ya zaidi ya Sh. milioni 23.3.

Mwezi uliopita, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (Ewura), ilitangaza kupandisha bei ya maji kwa asilimia 20 katika mji wa Moshi na miji ya jirani ya Hai na Moshi Vijijini ambako Muwsa inatoa huduma.

Kwa mujibu wa maofisa wa mamlaka hiyo ambao wanaendesha operesheni ya kuwakamata watumiaji batili, waliotumia nguvu kuchepusha njia kwenye miundombinu ya maji kwa lengo la kukwepa gharama za matumizi, wanatozwa faini na kisha kufunguliwa mashtaka.

Ofisa Uhusiano wa Muwsa, Dora Killo, aliwataja waliokamatwa kwa tuhuma hizo kuwa ni mmiliki wa eneo lenye kiwanda hicho, Godfrey Shayo, anayedaiwa kutumia maji kwa miezi 145 bila malipo.

Wengine ni Kimario Selema, mkazi wa Shanti mjini hapa ambaye ametozwa Sh. milioni 1.6 baada ya kutumia maji kwa miezi 33 na mkazi wa kijiji cha Chekereni-Weruweru.

 
CHANZO: NIPASHE