Na Herieth Makwetta, Mwananchi
Posted Jumatatu,Septemba16 2013 saa 12:52 PM
Posted Jumatatu,Septemba16 2013 saa 12:52 PM
Kwa ufupi
- Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy&Candy Records, Joe Kariuki alisema kampuni na mwanamuziki huyo anayependwa nchini Kenya ilitokea kutofautiana katika baadhi ya mambo hasa ubora wa kazi.
Nyota huyo aliyewahi kutamba na wimbo wa ‘Fagilia’, bado kazi zake zinaendelea kupendwa sehemu tofauti Duniani.
Dar es Salaam. Nguli wa muziki
aina ya ‘Takeu’ Lucas Mkenda ameingia katika mzozo mzito na meneja wake
mpya baada ya kutokukubaliana baadhi ya mambo aliyokuwa akishauriwa na
lebo hiyo mpya.
Mr Nice ambaye kwa sasa anamilikiwa na lebo ya
Candy&Candy Records kwa muda wa mwezi mmoja na nusu sasa baada ya
kutoka katika familia kubwa ya muziki ya GrandPa Recods, ameelezwa kuwa
alikuwa na mtazamo tofauti kibiashara na kampuni hiyo hali iliyotishia
kuvunjwa kwa mkataba wao.
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy&Candy Records, Joe Kariuki alisema
kampuni na mwanamuziki huyo anayependwa nchini Kenya ilitokea
kutofautiana katika baadhi ya mambo hasa ubora wa kazi.
“Mr Nice ni msanii anayependwa sana hasa Mombasa,
lakini wiki chache zilizopita tulikuwa na mabishano kidogo hii ilitokana
na mtazamo tofauti hasa ni kutokana na wimbo wake mpya wa ‘Akina Mama’
binafsi ule wimbo sikuupenda na nilimshauri kwamba ni vyema tungetumia
wimbo mwingine, lakini aling’ang’ania.
“Wimbo ule tuliupiga katika vyombo vya habari kwa bahati mbaya haukufanya vizuri lakini nilimtahadharisha mapema.
“Kampuni inaweza kupata hasara, lakini tumeamua
kuendelea na mkataba kwani kwa sasa ameelewa na tunakwenda kama kampuni
inavyotaka,” alisema Kariuki.
Kariuki anasema nyota huyo aliyewahi kutamba na
wimbo wa ‘Fagilia’ bado kazi zake zinaendelea kupendwa sehemu mbalimbali
nchini humo.
“Tukifika sehemu kama Malindi, Mombasa na maeneo
mengine mwanamuziki huyu bado ni chaguo la watu wengi. Anafanya vizuri
lakini bado kuna mengi yanayomtinga ila ‘akikaza buti’ hakika atarudi na
kuwa kama zamani hata Tanzania atashika chati za juu,” alisema.
Alisema muziki wa Bongo Fleva ni muziki pendwa
nchini humo ndiyo maana kampuni hiyo imeingia mkataba na wasanii wengi
kutoka nchini Tanzania wakiwamo Four - D, Top C, Mr Nice na Baby Madaha.
Wakati Mr Nice anaingia katika mgogoro huu mpya,
miezi michache iliyopita aliondolewa katika Kampuni kubwa ya muziki ya
GrandPa Records inayofanya kazi na wasanii wakubwa kama DNA, Ng’ang’a wa
Tusker Project Fame na wengine.
Mr. Nice alipigwa chini na kampuni hiyo ambayo
tayari ilikuwa imeshampigisha hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na
kumwandalia ziara ya kumtambulisha nchi nzima kwa lengo la kumwongezea
mashabiki, kumpa shoo ya kumtambulisha na kuachia wimbo mmoja aliofanya
na DNA uitwao ‘Tafuta’
GrandPa Records kupitia Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Refigah ilitoa tamko rasmi ambalo lilitaja sababu za kuachana na msanii huyo kwamba alikuwa ameshasaini mkataba na studio za Fishcrab chini ya Lamar na Sallam Sharaf. Wakati anasaini mkataba na GrandPa Records, hakuweka wazi.
SOURCE: MWANANCHI
GrandPa Records kupitia Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Refigah ilitoa tamko rasmi ambalo lilitaja sababu za kuachana na msanii huyo kwamba alikuwa ameshasaini mkataba na studio za Fishcrab chini ya Lamar na Sallam Sharaf. Wakati anasaini mkataba na GrandPa Records, hakuweka wazi.
SOURCE: MWANANCHI