Kwa ufupi
Mafanikio katika utunzaji wa hifadhi hii
umesababisha wanyama kama ngiri (warthogs) kuwa wengi na kuingia katika
makazi ya wananchi na kula kila wanachoweza kula bila kuogopa. Ni jambo
la kawaida. Kuna habari za hao ngiri kuishi na binadamu katika nyumba
moja, ngiri wakitumia makazi ya binadamu kuzaana.
Baada ya makala yangu ya wiki iliyopita baadhi
ya wasomaji walitaka kujua kama wangetembelea Sadani wangeona nini.
Katika Kijiji cha Sadani wananchi hawajaamka usingizini na kuitumia
mbuga ya wanyama kama fursa ya kiuchumi.
Awali nilidokeza kwamba kijiji hicho kina historia
ndefu, kama wananchi wangeamka basi utalii wa utamaduni na kihistoria
ungekuwa kivutio kikubwa sana kwa wageni ambao wangetaka kujifunza
historia hiyo.
Wageni wengi katika miaka iliyopita walifika
Sadani wakiwamo wachungaji wa Kijerumani Rebman na Krapf, na mpelelezi
na mwanajeshi mashuhuru, Sir Francis Burton, na safari za mwanzo za
waendeza dini ya Ukristo Tanzania Bara zilianzia Sadani, Pangani na hadi
Ubondei (Halle) na Kilimanjaro. Ushahidi huu utaupata kwenye vitabu
vyao wenyewe. Lakini ukifika Sadani utaona makaburi ya wageni waliofika
kutoka katikati hadi mwishoni mwa miaka ya 1800. Utaona ngome kubwa
iliyotumika kama soko la watumwa.
Lakini Kijiji cha Sadani kimezungukwa na mbuga ya
wanyama ya Sadani yenye kila aina ya wanyama. Mafanikio katika utunzaji
wa hifadhi hii umesababisha wanyama kama ngiri (warthogs) kuwa wengi na
kuingia katika makazi ya wananchi na kula kila wanachoweza kula bila
kuogopa. Ni jambo la kawaida. Kuna habari za hao ngiri kuishi na
binadamu katika nyumba moja, ngiri wakitumia makazi ya binadamu kuzaana.
Lakini cha ajabu mbuga ya wanyama ya Sadani ni ya
pekee. Hii ni mbuga ya kwanza katika Tanzania ambayo imetoka bara hadi
baharini.
Kasa hao huzaliwa hapo na kusambaa maeneo ya
mbali, hasa Australia. Lakini wakati wa kuzaana huja tena hapohapo bila
kupotea. Hiki ni kivutio cha aina yake. Sadani ilianzishwa miaka ya 1950
kama ranchi ya serikali ya mkoloni wakati huo kwa ajili ya ng’ombe. Na
ukifika kijijini Mkwaja Ranchi utaona ushahidi huo wa kihistoria. Kuna
mengi ya kuona ingawa maelezo katika maandishi hakuna.
Ckayoka28@yahoo.com, 0766959349
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI