Kwa ufupi
- Zaidi ya watu 3000 waliuawa
Taifa la Marekani jana limetimiza miaka 12 tangu
Septemba 11, mwaka 2001, yalipotokea mashambulizi ya kigaidi kwenye
miji ya New York na Washington DC .
Mashambulizi hayo yalisababisha watu takribani
3,000 kupoteza maisha na kuliweka taifa hilo kwenye majonzi mazito ya
kupotelewa na wapendwa wao.
Kutokea kwa mashambulizi hayo kuliacha mshangao
mkubwa kwa Taifa la Marekani ambalo lilidhaniwa kuwa lipo imara
kiusalama na lisingeweza kushambuliwa kwenye ardhi yake kama
ilivyotokea.
Hali ilivyokuwa
Tukio hilo lilipotokea Jiji la New York na
Washington DC, anga lilionekana kuchafuka kwa moshi wakati ndege mbili
za abiria zilizotekwa zilipogonga katika minara ya majengo ya biashara
(World Trade Center ). Ndege nyingine ziligonga kwenye makao makuu ya
Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon. Tukio hilo kwa ujumla lilizua
mshangao mkubwa duniani kutokana na imani ya wengi kwamba Marekani ni
taifa kubwa na lenye ulinzi imara.
Ndege nyingine watekaji walidhibitiwa
Katika hatua nyingine ndege ya nne iliyotekwa
ilianguka karibu na mji mdogo wa Shanksville, Pennsylvania, baada ya
abiria kupambana na watekaji na kuchukua udhibiti wa ndege hiyo.
Taifa hilo tajiri duniani baadaye lilibadili idara
zake za ulinzi wa ndani na kubadili sheria ili kuzuia uwezekano wa
mashambulizi mengine kama hayo kutokea.
Al Qaeda yahusishwa.
Tukio hilo kubwa kutokea duniani liliwahusisha wafuasi wa mtandao wa al Qaeda .
Serikali ya wakati huo ilikuwa inaongozwa na Rais
mstaafu George Bush, baada ya kutokea kwa tukio hilo mtandao wa al
Qaeda ulihusishwa na mashambulio hayo moja kwa moja.
Kumtafuta Osama
Baada ya Serikali ya Marekani kuihusisha al Qaeda, iliamua
kuivamia nchi ya Afghanistan na Iraq na kuzishambulia nchi hizo kwa
lengo la kumsaka kiongozi wa Al Qaeda Osama Bin Laden ambaye ndiye
aliyehusishwa kupanga njama za kuishambulia Marekani.
Hata hivyo tokea wakati huo ilikuwa ikijulikana
kuwa Al Qaeda ni kundi lililoundwa na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA
muongo mmoja kabla ya hapo wakati wa vita dhidi ya majeshi ya Urusi ya
zamani nchini Afghanistan.
Viongozi wakuu wa kundi hilo hususan ukoo wa Bin
Laden ulikuwa na uhusiano wa karibu wa kibiashara na baadhi ya wanasiasa
nchini Marekani wakiwemo wa ukoo wa Bush.
Jambo hilo lilisababisha baada ya kutokea kwa
tukio hilo Septemba 11.Mashambulizi ya maneno dhidi ya Osama Bin Laden
yaliyofuatiwa na uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan.
Tangu Marekani ilipoivamia Afghanistan, wasomi
wa Marekani walieleza bayana kuwa sera za uingiliaji wa kijeshi za
Serikali zilizopita, ndizo zilizosababisha kutokea matukio ya umwagaji
damu ya Septemba 11.
Kwa mtazamo wa wasomi na wanafikra hao, kama
Serikali zilizopita nchini Marekani zisingeunga mkono ukiukaji wa wazi
wa misingi ya demokrasia na haki za binadamu katika pembe mbalimbali
duniani na kusababisha maafa kadhaa wakati wa vita ya Ghuba ya Uajemi ya
mwaka 1991, huenda magaidi wasingehangaika na Marekani.
Obama anakumbuka
Wakati Wamarekani wanakumbuka na kuadhimisha siku
hiyo, Rais wa Marekani Barack Obama ametembelea maeneo yote ambayo
mashambulizi yalitokea.
Katika hotuba yake ya kila wiki alisifu watu
waliofanya kazi za uokoaji ambapo walijaribu kuokoa maisha ya wahanga
wakati wa mashambulizi hayo.
Mapema mwaka huu, vikosi maalum vya Marekani
vilifanikiwa kumwua kiongozi wa Al-Qaida Osama bin Laden huko Pakistan
na kutimiza ahadi aliyoitoa rais wa zamani wa Marekani George W. Bush.
Hakuna hotuba
Kwa mara ya kwanza kwenye maadhimisho ya tukio hilo hakukuwepo na hotuba yoyote wakati wa sherehe hizo kutoka
Familia za zaidi ya watu waliouawa ziliruhusiwa kufika katika
eneo la tukio la mashambulizi hayo maarufu kama Ground Zero mjini New
York,.
Awali idara ya afya nchini Marekani ilitangaza
kuwa manusura wa mashambulio hayo na wale waliowasaidia watapewa
uchunguzi na matibabu ya takriban aina hamsini za saratani bila malipo,
kwa sababu walivuta hewa iliyokuwa na sumu baada ya mashambulio hayo.
Makala hii imeandikwa na, Aidan Mhando kwa msaada wa Mashirika mbalimbali ya habari
SOURCE: MWANANCHI
kwa wanasiasa.SOURCE: MWANANCHI