Monday, 2 September 2013

Uvimbe katika mfuko wa uzazi (1)

Posted  Jumapili,Septemba1  2013  saa 14:0 PM
Kwa ufupi
Tafiti nyingi zinaonyesha wanawake wa asili ya Kiafrika wanapata zaidi tatizo hili kuliko wazungu.


Hujulikana kwa lugha ya kigeni kama uterine myoma, fibroid. Ni wazi kwamba tatizo hili linawakumba zaidi wanawake.
Huwapata kwa asilimia tano wanawake wenye umri kati ya miaka 20 hadi 30, asilimia karibu 20 kwa wenye umri kati ya miaka 30 hadi 40, na zaidi ya asilimia 40 kwa wale wenye umri zaidi ya miaka 40.
Hii inamaanisha kwamba kadiri umri unavyokuwa umkubwa mwanamke ana nafasi kubwa ya kupata ugonjwa huu, pia nitatizo kubwa katika jamii kwa sasa, ikizingatiwa kwa ukubwa kwamba inahusu mfuko wa uzazi.
Pia utaona kwamba huwakumba zaidi kina mama ambao wako katika umri wa kuweza kuzaa (reproductive age).
Uvimbe huwa wa saizi mbalimbali, huanza kuwa mdogo, na baadaye kuwa mkubwa sana na mwanamke kuonekana kama anatumbo la uzazi (mjamzito).
Uvimbe huu unaweza kuwa mmoja lakini wakati hutokea uvimbe zaidi ya mmojaamboa hutanda katika mfuko wa uzazi.
Tafiti nyingi zinaonyesha wanawake wa asili ya Kiafrika wanapata zaidi tatizo hili kuliko wazungu.
Huwapata pia zaidi wanawake ambao hawajazaa kabisa, kubahatika kutunga mimba na kuzaa (Nulliparity), wanawake wanene, au kuwepo kwa ndugu wa karibu aliyepatwa na ugonjwa huu mfano mama na dada.
Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kutokwa damu nyingi sana kwa muda mrefu wakati wa hedhi ikiambatana na mabonge mabonge isivyo kawaida.
Dalili nyingine ni kupata maumvi ya kiuno, ugonjwa kubana viungo vingine vya mwili (pressure symptoms) hivyo kupumua kwa shida au kukojoa mara kwa mara au kushindwa kupata choo kikubwa kawaida. Nyingine ni pamoja na kutokutunga mimba, au mimba kuharibika na kutoka.
Uchunguzi
Nirahisi kwa mtaalamu kugundua ugonjwa huu au uvimbe katika mfuko wauzazi kwa kumkagua, au kumpima mgojwa (bimanual examination).
 Itaendelea wiki ijayo...

source: Mwananchi