Friday, 20 September 2013

Waziri Nchimbi aitaka Polisi ZNZ kuhakikisha wahalifu wa tindikali wanapatikana


 Waziri wa mambo ya ndani ya nchi  Dk. Emmanuel Nchimbi ameliambia jeshi la polisi kuwa serikali haikubali kuona wahalifu wa tindikali bado wako mitaani hivyo ametoa agizo la kutafutwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa wahalifu wote wa tindikali.
Dk. Nchimbi ametoa agizo hilo hapa  Zanzibar wakati alipokutana na makamanda na askari wa mikoa mitatu ya Unguja katika ukumbi wa makao makuu ya polisi Ziwani ambapo amesema kwa gharama yeyote wahalifu hao wasakwe na watafutwe  na serikali zote mbili haziridhiki kuona wahalifu hao wanatamba  mitaani.
Katika mkutano huo ulihudhuriwa na waziir wa nchi afisi ya rais tawala za mikoa na vikosi vya SMZ Mh Haji Omar Kheir ambaye amesema vitendo hivyo ni dalili ya kutaka kuwepo kwa uvunjaji wa amani na kuwataka askari hao kutotumia kigezo cha kukosa haki zao kuwa ni sababu ya kushindwa kuwakamata wahalifu..
Katika mkutano huo  askari hao kutoka mikoa ya Mjini Magharibi,kusini na kaskazini walipata fursa ya kushauri na kuelezea matatizo yao ikiwemo ya afya lakini pia kuhusu udhibiti wa uhalifu nchini.
Zanzibar imeshuhudia matukio  saba ya uhalifu wa tindikali  lakini jeshi la poliis hadin sasa limeshindwa kuwafikisha wahusika mahakamani.

SOURCE: ITV-DAIMA