Wednesday 4 September 2013

Ada za magari kulipwa kwa M-pesa


Na Newstar Rwechungura na Benjamini Mwangoka  (email the author)

Posted  Jumanne,Septemba3  2013  saa 21:12 PM
Kwa ufupi
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema M-pesa imeleta urahisi zaidi kwa mamlaka ya mapato katika ukusanyaji wa ada za magari.


Dar es Salaam. Kampuni ya Simu za Mikononi Vodacom kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imezindua mfumo wa ulipaji ada za magari kupitia huduma ya M-Pesa.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa Vodacom,Kelvin Twissa alisema jana kuwa ulipaji huo utawaepusha Watanzania kukumbana na foleni zisizo za lazima wakati wa ulipaji wa ada za magari.
“Ni wakati mwingine M-pesa inawapa walipakodi na wananchi utaratibu mwepesi na salama, huku wakiwa na uhakika wa kulipa ada za leseni ya magari kwa urahisi wakati wowote” alisema
Alisema Vodacom itaendelea kuuwezesha mfumo wa M-pesa kuwa wenye kutoa suluhisho la masuala mengi ili kukidhi matarajio ya kampuni hiyo ya kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema M-pesa imeleta urahisi zaidi kwa mamlaka ya mapato katika ukusanyaji wa ada za magari.
Alisema TRA ina imani kuwa ushirikiano wake na Vodacom utakuwa wenye tija zaidi katika siku zijazo kwa kuhakikisha mfumo wa M-pesa unatoa uwezo kwa walipakodi.
Aliongeza kuwa inakadiriwa kuwa kwa kipindi cha wiki mbili TRA imekusanya kiasi cha Sh2 bilioni ikiwa ni makusanyo kutoka M-pesa  pekee

source; Mwananchi