Na Daniel Mjema,Mwananchi
Posted Septemba21 2013 saa 9:37 AM
Posted Septemba21 2013 saa 9:37 AM
Kwa ufupi
Operesheni hiyo iliyopewa jina la “Operesheni
Mathayo Out” kwa kifupi OMO ilianza wiki iliyopita kwa kufanya mikutano
ya hadhara jimboni humo na itaendelea tena wiki ijayo.
Same. Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), kimetangaza operesheni maalumu ya kumng’oa ubunge, Mbunge wa
Jimbo la Same Magharibi, Dk David Mathayo David katika Uchanguzi Mkuu wa
2015.
Operesheni hiyo iliyopewa jina la “Operesheni
Mathayo Out” kwa kifupi OMO ilianza wiki iliyopita kwa kufanya mikutano
ya hadhara jimboni humo na itaendelea tena wiki ijayo.
Mmoja wa makamanda wa operesheni hiyo, Gervas
Mgonja alisema jimbo hilo limekuwa chini ya himaya ya CCM tangu Uhuru
lakini wananchi wake wapo kama wamefunga ndoa na tatizo la maji.
Dk Mathayo ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Uvuvi alipoulizwa kuhusu operesheni hiyo ya kumng’oa alisema,
Chadema ni chama kidogo na hakimnyi usingizi kwa madai uwezo wa kampeni
unaishiSOURCE: MWANANCHI