Na Tausi Ally
Posted Jumatano,Septemba11 2013 saa 22:4 PM
Posted Jumatano,Septemba11 2013 saa 22:4 PM
Kwa ufupi
Washtakiwa hao wataanza kujitetea kuanzia
Oktoba 16,17,18,24 na 25, mwaka huu na kudai kuwa watajitetea kwa njia
ya kiapo na kwamba watakuwa na mashahidi 13.
Dar es Salaam.Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
imesema kuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Ardhi na
Maendeleo ya Makazi, Simon Lazaro na wenzake wawili wana kesi ya kujibu
kuhusiana na matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa Sh100 milioni.
Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana alisema jana baada
ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande wa mashtaka
pamoja na vielelezo 15 walivyoviwasilisha mahakamani hapo, amewaona
washtakiwa wote wana kesi ya kujibu hivyo wanatakiwa kuanza kujitetea.
Washtakiwa hao wataanza kujitetea kuanzia Oktoba
16,17,18,24 na 25, mwaka huu na kudai kuwa watajitetea kwa njia ya kiapo
na kwamba watakuwa na mashahidi 13.
Mbali na Lazaro, washtakiwa wengine wanaokabiliwa
na kesi hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Matumizi Bora ya Ardhi,
Gerald Mango na Kaimu Mhasibu Mkuu wa tume hiyo, Charles Kijumbe. Kesi
hiyo inasomwa huku Lazaro akiwa ni Mkurugenzi kamili katika idara hiyo.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI