Na Zainab Maeda
Posted Alhamisi,Septemba12 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Septemba12 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Alisema baada ya kazi hiyo, watu hao walianza
kunywa pombe ya kienyeji na ilipofika jioni watu 19 walipatwa na ugonjwa
wa tumbo. Kamanda huyo alisema baadaye watu hao walipelekwa katika
Zahanati ya kijiji hicho kwa matibabu.
Iringa. Zaidi ya watu 19 katika Kijiji cha
Imega, katika Wilaya ya Kilolo, wamenusurika kufa baada ya kunywa pombe
ya kienyeji inayodhaniwa kuwa na sumu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani
Mungi alisema tukio hilo lilitokea juzi wakati watu hao walipokwenda
kuhudhuria sherehe iliyoandaliwa na mzee mmoja. Kwa mujibu wa kamanda
huyo, sherehe hizo zilikuwa ni za kumuaga binti yake aliyekuwa akiolewa.
Alisema baada ya kazi hiyo, watu hao walianza
kunywa pombe ya kienyeji na ilipofika jioni watu 19 walipatwa na ugonjwa
wa tumbo. Kamanda huyo alisema baadaye watu hao walipelekwa katika
Zahanati ya kijiji hicho kwa matibabu.
Alisema wakati wakiendelea kupata matibabu ,mmoja
wa watu hao, alizidiwa na kukimbizwa katika Hosptali ya Itunda kwa
matibabu zaidi. Alisema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa huenda pombe
walioitumia ilikuwa na sumu.
“Pombe hiyo inatokana na mahindi na inasemakana mahindi hayo yalikuwa na dawa. Tunafanya uchunguzi,” alisema Mungi.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI