Na Rachel Chibwete
Kwa ufupi
Kato alisema, wakulima wengi wa zabibu mkoani Dodoma, wameitikia wito wa kulima zao la zabibu lakini tatizo ni kukosa soko.
Dodoma. Uzalishaji wa zabibu sasa umekuwa mkubwa
kuliko uwezo wa viwanda vinavyotengeneza mvinyo nchini,jambo
linalosababisha wakulima kukosa soko la zao hilo.
Hayo yalisemwa na Meneja wa Kiwanda cha
Kutengeneza Mvinyo cha Alko Vintages, Archard Kato alipokuwa akizungumza
na gazeti hili ofisini kwake juzi.
Kato alisema, wakulima wengi wa zabibu mkoani Dodoma, wameitikia wito wa kulima zao la zabibu lakini tatizo ni kukosa soko.
Alisema hiyo inasababishwa na viwanda kuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha mvinyo na nafasi ya kutunzia bidhaa zinazozalishwa.
“Inauma kuona wakulima wanakosa soko la mazao
lakini hata sisi wadau, hatuna cha kufanya kwa sababu uwezo wetu wa
kuzalisha ni mdogo kutokana na mashine tulizonazo,” alisema kato.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI