Na Beatrice Moses, Mwananchi
Posted Septemba14 2013 saa 9:41 AM
Posted Septemba14 2013 saa 9:41 AM
Kwa ufupi
Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema
soko la ajira kwa Watanzania linakabiliwa na hatari ya kushuka kutokana
na Serikali kushusha viwango vya ufaulu kwa wanafunzi wanaojiunga na
vyuo vya elimu ya juu.
Sumaye aliyasema hayo jana kwenye mahafali ya
darasa la saba katika Shule ya Msingi New Era Montessory, iliyopo nje
kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kushusha kiwango cha wanafunzi kujiunga na
elimu ya juu si dawa ya kusaidia wengi kuweza kupata elimu hiyo bali ni
kuporomosha viwango vya elimu nchini.
“Mteremko katika elimu nchini udhibitiwe kwa
sababu unaweza kusababisha Watanzania wenye shahada kukosa ajira. Huko
ni kushindwa kushindana katika soko la ajira ‘alisema.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI