Kwa ufupi
Serikali yakanusha taarifa zinazodai kuwa mke
wa Rais, Salma Kikwete ni ndugu wa kiongozi wa zamani wa Rwanda, Juvenal
Habyarimana
Dar es Salaam. Uhusiano kati ya
Tanzania na Rwanda unazidi kudorora kutokana vyombo vya habari na
baadhi ya maofisa wa nchi hiyo kuanza ‘kuichokonoa familia ya Rais
Jakaya Kikwete’.
Tovuti ya News of Rwanda, imedai kuwa mke wa Rais,
Salma Kikwete ni ndugu wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo, Juvenal
Habyarimana ambaye aliuawa kwenye ajali ya ndege wakati akitokea nchini
Tanzania mwaka 1993.
Madai hayo yametokana na mtandao wa Wiki Leaks,
ambao ulinasa mawasiliano kati ya Ubalozi wa Marekani nchini na Serikali
ya nchi hiyo. Kadhalika taarifa hiyo ya Wiki Leaks imenukuliwa na
magazeti mengine ya Rwanda likiwamo gazeti maarufu la New Times.
Hata hivyo, Msemaji wa Serikali ambaye ni
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene amekanusha
taarifa hizo zinazodai kuwa Rais Kikwete ni shemeji yake na Habyarimana.
“Taarifa hizi hazina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Kikwete,” alisema Mwambene.
Mwambene amefafanua kuwa lengo la mitandao ya
kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma na si kupotosha jamii kwa
kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
Kutokana na tovuti hiyo kuchapisha habari hiyo, wasomaji wake walitoa maoni mengi ya kumkashifu Rais Kikwete.
Baadhi yao walikwenda mbali zaidi kwa kuhusisha
habari hiyo na uamuzi wa hivi karibuni wa kuwatimua raia wa Rwanda
wanaoishi bila kibali nchini.
“Kama Mama Salma Kikwete ni binamu wa Habyarimana
basi Rais Kikwete amrudishe nyumbani kwao Rwanda,” aliandika msomaji wa
gazeti hilo, Osma Kanyambo.
Hali hiyo ni mwendelezo wa vita vya maneno kati ya Tanzania na Rwanda, ambavyo vilianza tangu mwezi uliopita.
Chanzo cha hali hiyo ni ushauri uliotolewa na Rais
Kikwete wa kuitaka Rwanda kuzungumza na kundi la waasi la FLDR ambalo
limekuwa likiendesha vita kwa miaka 16 sasa wakiwa mafichoni katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Rais Kikwete katika hotuba ya mwisho wa mwezi
uliopita alikiri kudorora kwa uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda na
kwamba nchi hiyo inamshutumu kutokana na ushauri aliowapa.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi
hiyo, Louis Mushikiwabo walikaririwa kwa nyakati tofauti wa wakitoa
kauli zenye mwelekeo wa kashfa kwa Rais Kikwete.
Hali imekuwa mbaya zaidi baada ya Rais Kikwete
kuagiza operesheni ya kuwaondoa raia wa nchi jirani (Rwanda ikiwamo)
wanaoishi nchini bila ya vibali.
Serikali ya Rwanda pekee ndiyo imepinga operesheni
hiyo, ambayo imesababisha kuondolewa kwa raia wake wapatao 6,000 ambao
walikuwa wakiishi nchini kinyume cha sheria. Nchi nyingine; Burundi,
Uganda na DRC ambazo pia raia wake wameondolewa lakini hazikulalamikia
operesheni hiyo.
Taarifa ya Weak Leaks
Taarifa hiyo ni ile iliyotumwa na ofisa mwandamizi
wa Ubalozi wa Marekani nchini, Shabyna Stillman Mei 5, 2005 akidai kuwa
Mama Salma ni binamu wa Habyarimansource: Mwananchi