Kwa ufupi
Bunda. Diwani wa Kata ya Kisorya wilayani hapa,
Misana Jigwira (CCM), amesema yuko tayari kuachia nafasi yake kwa
kujiuzulu, iwapo mganga mkuu mfawidhi wa kituo cha afya cha kata hiyo
hatahamishwa kazi.
Jigwira alisema atachukua hatua hiyo kutokana na
mganga huyo, kutokuwajibika ipasavyo, ikiwa ni pamoja na kutokuwapatia
dawa wagonjwa wanaofika kituoni hapo licha ya kuchangia fedha papo kwa
papo kiasi cha Sh1,000 kwa kila mgonjwa na kwamba kwa sasa fedha hizo
zimeongezeka na kufikia Sh3,000.
Diwani huyo bila kutafuna maneno alisema licha ya
wagonjwa hao kuchangia fedha hizo, huambiwa na mganga huyo kwamba dawa
hazipo na kuwaagiza waende kununua kwenye maduka ya watu binafsi.
Alisema kutokana na kero hiyo wananchi wamekuwa
wakifika kwake mara kwa mara kulalamikia hali hiyo, ikiwa ni pamoja na
huduma duni wanazopata kwenye kituo hicho.
source: Mwananchi
source: Mwananchi