Wednesday 25 September 2013

Maria; Anaishi na waume wawili nyumba moja

Posted  Jumapili,Septemba22  2013  saa 14:25 PM
Kwa ufupi
Uhusiano wao ulianza kuingia doa mwaka 2006. “Paul aliondoka kwa miezi sita kikazi na kuacha upenyo katika uhusiano wetu, nilianza uhusiano na meneja wangu mpya, Peter.”

London. Maria Vogel (33), mwenye asili ya Zimbabwe katika mji wa Bulawayo amejikuta akiishi na mume wake wa ndoa na hawara yake katikam nyumba moja baada ya kila mmoja kukataa kuachana naye.
Hivi sasa Maria anaishi na familia yake akiwa na wanaume hao Paul Butzki na Peter Gruman, huko Barking jijini London pamoja na binti zake wawili Laura, 16 na Amy, 12.
“Miezi 15 sasa tunaishi pamoja , tunapendana na kulea watoto kama wazazi wengine, ninakuwa na muda wa kukaa na kila mmoja kwa ratiba,”anasema Maria.
Akizungumza na gazeti la Daily Monitor Maria alisema kuwa alikutana na Paul ambaye ni mumewe alipokuwa akisoma sekondari huko Northlea wakati huo alikuwa na umri wa miaka 15 na miaka miwili baadaye alijifungua binti yake Laura. Uhusiano wao ulianza kuingia doa mwaka 2006. “Paul aliondoka kwa miezi sita kikazi na kuacha upenyo katika uhusiano wetu, nilianza uhusiano na meneja wangu mpya, Peter.”anasimulia akiongeza:
“Tulianza kukutana na Peter wakati wa chakula cha mchana baadaye tuliishia kuwa wapenzi. miezi michache baadaye akaamua kuachana na mkewe, niliendelea kuwa karibu naye mpaka mwaka 2010, nilipoona siwezi tena kujificha nilimweleza mume wangu na kuondoka kwenda kuishi na Peter. Sikupenda familia yangu ilipokuwa ikinililia hasa mume wangu. Mwaka 2012 Peter na Paul walikuwa marafiki, ndipo walipoamua kuwa tunaweza kuishi pamoja bila matatizo.”
Imeandaliwa na Herieth Makwetta

SOURCE: MWANANCHI