Tuesday 10 September 2013

Mtanda aibuka kidedea

Posted  Jumatatu,Septemba9  2013  saa 22:36 PM
Kwa ufupi
Akitangaza matokeo ya uchagunzi huo, Chikawe alisema Buriani amepata kura 316 na Mtanda ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga, amepata kura 1002.


Lindi. Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM katika Wilaya ya Lindi, wamemchagua kwa mara nyingine Saidi Mtanda kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM baada ya kumshinda mpinzani wake, Shaibu Buriani kwa kura 600.
Uchaguzi huo ulifanyika juzi katika Kijiji cha Kiwalala na kusimamiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Abdalah Chikawe.
Akitangaza matokeo ya uchagunzi huo, Chikawe alisema Buriani amepata kura 316 na Mtanda ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga, amepata kura 1002.
Mbunge wa Mtama, Benard Membe, aliwataka wajumbe kutumia hekima kuchagua kiongozi anayefaa.
Membe alisema CCM wilayani humo, inahitaji viongozi walio tayari kujitoa kwa ajili ya chama.
Uchaguzi huo umerudiwa baada ya CCM kupokea rufaa na kutengua matokeo ya ule wa wali, uliokuwa umelalamikiwa na Buriani (Mwanja Ibadi)

source: Mwananchi