Wednesday 25 September 2013

Picture: Al Shabaab walitangaza matayarisho ya kushambulia Kenya, na idadi ya vifo miezi miwili iliyopita! (Al Shabaab informed the public about their plan to attack on 19.Jul, 2013


Msemaji wa al Shabaab, Sheikh Ali Mohamud Rage
Msemaji wa al Shabaab, Sheikh Ali Mohamud Rage

Website maarufu ya teknolojia nchini Kenya, TechMtaa, wamefichua kuwa al Shabaab walitangaza hadharani mipango ya kushambulia Kenya na kuhakikisha idadi ya vifo vitakavyotokea miezi miwili iliyopita kwa kinachoonekana kama kuashiria shambulio la Westgate Mall.

Al Shabaab walitangaza dhamira yao hiyo kwa kupitia akaunti yao ya Twitter, HSMPress_. Herufi HSM zinasimama kwa jina kamili la kundi hilo, “Harakat al-Shabaab al-Mujahideen.”
Bado haijulikani kama vyombo vya dola nchini Kenya vilikua vinafahamu kuwepo kwa taarifa hiyo na kama walichukulia serious.
Tafsiri ya tweet hiyo ni: “shambulio la kustaajabisha la al Shabaab tunalohakikisha litasababisha vifo zaidi ya 50 na kutangazwa na vyombo vya habari kwa undani lipo katika hatua za mwisho za matayarisho. Lifanyike Kenya au Somalia? Godane* anajiuliza.” [ *Ahmad Abdi Godane ni kiongozi mkuu wa al Shabaab]

Kama umeshindwa kuona tweet hapo juu, hii hapa chini ni picha ya screen ya tweet hiyo, tarehe ikionyeshwa na mshale mwekunduA mother and her children hide from gunmen at Westgate Shopping Centre in Nairobi