Wanaharakati
wapatao 18 wametembea kwa miguu kutoka jijini Arusha hadi Dar es
salaam wakiitaka serikali kuchukua hatua za dhati dhidi ya uwindaji
haramu wa tembo.
Wakizungumza
na waandishi wa habari baadhi ya wanaharakati hao wamesema
vitendo vya kuuwa kwa tembo vinawasikitisha na hivyo wanataka
kila mtu pamoja na serikali wachukue hatua kudhibiti hali hiyo
Naye
mwenekiti wa kamati ya bunge ardhi mazingira na maliasili Mh James
Lembeli ameonyesha kukerwa na vitendo vya baadhia ya magari ya
serikali kukamatwa yakiwa yamebeba pembe za ndovu na huku wahuska
wakiwa hawachukuliwi hatua zozote
Akipokea
na kuhitimisha matembezi hayo naibu waziri wa maliasili na utalii Mh
Lazaro Nyalandu amesema tatizo la ujangili ni kubwa kuliko watu
wanavyodhani na hivyo ameaahidi kuwa serikali itawasaka wale wote
wanaohusika na kuwachukulia hatua.source: ITV-DAIMA