Kwa ufupi
Akisoma maelezo ya awali, Ndimbo alidai kuwa
kati ya Aprili na Mei, 2012, mshtakiwa alijitambulisha kwa Dk Slaa, Lema
na Profesa Safari kuwa yeye ni mtumishi wa Takukuru.
Hai. Jaji Mkuu Mstaafu,Barnabas Samatta ni
miongoni mwa mashahidi 12 watakaotoa ushahidi katika kesi ya jinai ya
jaribio la kumtapeli Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willbrod Slaa.
Wengine watakaotoa ushahidi katika kesi hiyo
inayomkabili Abedi Adam Abedi (22) ni Dk Slaa mwenyewe na Mbunge wa
Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema.
Orodha ya majina ya mashahidi hao ilitolewa
mahakamani juzi mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Hai, Denis Mpelembwa
na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Maghela Ndimbo.
Wengine watakaotoa ushahidi ni wakili mashuhuri wa
Chadema, Profesa Abdalah Safari, Rumisha Slaa, Happynes Masue, Godfrid
Njau, Gervas Geneya, Neema Godbless,Aron Misanga, Prosper Mbilinyi na
Judith Mashashi.
Akisoma maelezo ya awali, Ndimbo alidai kuwa kati
ya Aprili na Mei, 2012, mshtakiwa alijitambulisha kwa Dk Slaa, Lema na
Profesa Safari kuwa yeye ni mtumishi wa Takukuru.
Ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, mshtakiwa
aliwapigia simu Dk Slaa, Lema na Profesa Safari na kujitambulisha kuwa
yeye ni Abel Kibaso Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Ulanga.
Katika kipindi hicho pia, mshtakiwa aliwapigia
simu viongozi hao akijitambulisha ni Jaji mstaafu Samatta akitaka wampe
pesa ili washinde katika kesi iliyokuwa mahakama ya Rufaa.
Rufaa hiyo namba 47/2012 ilifunguliwa na Lema
dhidi ya Mussa Hamisi na wenzake akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Arusha
ya kupinga kuvuliwa Ubunge wa Arusha mjini kesi ambayo kwa sasa
ilishatolewa uamuzi.
mashtaka huyo alidai mahakamani kuwa mshtakiwa
alijifanya ni Jaji Mkuu Mstaafu Samatta wakati akijua siyo Jaji Samatta
kwa lengo tu la kujipatia fedha kinyume cha sheria.
Hata hivyo Lema alishinda Rufaa hiyo na kurudishiwa Ubunge wake.
Mshtakiwa amekanusha mashtaka hayo na kesi hiyo
imepangwa kuanza kusikilizwa rasmi Septemba 25 ambapo Jaji Samatta ni
miongoni mwa mashahidi wa upande wa Jamhuri.
chanzo: mwananchi
chanzo: mwananchi