Na Mwandishi Wetu,
Posted Ijumaa,Septemba27 2013 saa 24:0 AM
Posted Ijumaa,Septemba27 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
Shambulio hilo ni la pili kufanyika kwenye
maeneo mawili tofauti ndani ya saa 24, baada ya lingine lililofanyika
kwenye Mji wa Wajir, muda mfupi baada ya taarifa za kudhibitiwa kwa watu
wanaodhaniwa kuwa magaidi walioshambulia jengo la kibiashara la
Westgate mjini Nairobi.
Nairobi. Wakati Serikali ya
Kenya imeliomba Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) kumkamata
Mwingereza Samantha Lewthwaite (pichani), taarifa zinadai kuwa mwanamke
huyo alipitia mpaka wa Namanga, Arusha kwenda Nairobi ambako anahusishwa
na tukio la ugaidi.
Lewthwaite, ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Mjane mweupe’ inaaminika anashirikiana na kundi la magaidi la Al-Shabab la Somalia.
Kundi hilo ndilo linaaminika lilihusika na mashambulizi kwenye jengo la Westgate jijini Nairobi, wikiendi iliyopita.
Hata hivyo, taarifa ya Interpol ilisema kuwa
alikuwa anatakiwa kujibu mashtaka ya kumiliki mabomu na kupanga njama za
ugaidi Desemba 2011.
Interpol haikuhusisha maombi hayo ya Serikali ya Kenya na mashambulizi ya Nairobi.
Pia Lewthwaite inasemekana aliingia nchini humo kwa kutumia mpaka wa Tanzania.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Afrika ya Kusini,
vinasema mwanamke huyo alitumia pasi ya kusafiri ya nchi hiyo kuingia
Kenya kwa kutumia mpaka wa Namanga uliopo mkoani Arusha.
Taarifa hizo zinasema mwanamke huyo alitumia mpaka
wa Lunga Lunga na Namanga kati ya Februari na Agosti mwaka 2011
akitumia jina la Webb.
Habari hizo zinaeleza kuwa, awali mwanamke huyo
alikuwa anaishi Afrika Kusini ambako aliweza kukopeshwa fedha benki na
kuweza kupanga sehemu ya kuishi.
Wakati huohuo, watu wanaodhaniwa kuwa magaidi
wamefanya shambulio kwenye Kituo cha Polisi mjini Mandera na kuua askari
wawili, kujeruhi watatu kisha kuchoma zaidi ya magari 11 jana asubuhi.
Shambulio hilo ni la pili kufanyika kwenye maeneo
mawili tofauti ndani ya saa 24, baada ya lingine lililofanyika kwenye
Mji wa Wajir, muda mfupi baada ya taarifa za kudhibitiwa kwa watu
wanaodhaniwa kuwa magaidi walioshambulia jengo la kibiashara la Westgate
mjini Nairobi.
Shambulio hilo limefanyika wakati kikosi maalumu
cha wataalamu wa mabaki ya mabomu wa Kenya na wale wa kimataifa kikianza
kufanya upekuzi wa jengo hilo, ili kubaini wahusika halisi wa shambulio
hilo na aina ya silaha zilizotumiwa.
arifa za awali zilieleza kwamba inadhaniwa waliofanya mashambulizi hayo ni sehemu ya wavamizi hao wanaodaiwa kutoroka, ikiwa ni mkakati wa kuvizubaisha vyombo vya usalama ili kuwawezesha wenzao kutoroka bila vikwazo.
arifa za awali zilieleza kwamba inadhaniwa waliofanya mashambulizi hayo ni sehemu ya wavamizi hao wanaodaiwa kutoroka, ikiwa ni mkakati wa kuvizubaisha vyombo vya usalama ili kuwawezesha wenzao kutoroka bila vikwazo.
Uvamizi wa jengo la ghorofa nne la Kituo cha
Kibiashara cha Westgate uliofanyika Jumamosi iliyopita na watu
wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Kundi la Al Shabaab na kudumu kwa siku nne
ulisababisha vifo vya watu 62 na wengine zaidi ya 150 kujeruhiwa, kwa
mujibu wa taarifa ya Serikali ya Kenya.
Katika shambulio hilo la Kituo cha Polisi Mandera, magari saba kati ya 11 yameharibiwa vibaya kiasi cha kutokutambulika.
Taarifa ya polisi ilieleza kwamba waliofanya
shambulio hilo walirusha bomu la roketi (RPG) na kusambaratisha ofisi ya
mkuu wa kituo hicho, kisha kutoweka saa 10 alfajiri jana.
Mkuu wa Polisi Eneo la North East aliyemaliza muda
wake, Charlton Mureithi alisema watu hao waliwavamia askari polisi
waliokuwa wamelala kwenye jengo la utawala.
“Wamesababisha madhara makubwa ikiwemo vifo vya maofisa wetu kisha wakatoroka, lakini tunaamini watakamatwa,” alisema.
Wanadaiwa kutumia muda wao kwenye kituo hicho baada ya kuvamia na kuwafyatulia risasi maofisa hao wa polisi wakiwa karibu.
Walishambulia kwa bomu na kuyalipua kwa kutumia petroli magari yaliyokuwa yameegeshwa kwenye kituo hicho.
Maofisa wa polisi waliojeruhiwa walifikishwa hospitalini mjini Nairobi mchana wa jana kwa ajili ya matibabu zaidi.
Shambulio hilo ni la pili kufanyika ndani ya siku
moja baada ya lingine lililofanyika kwenye Mji wa Wajir juzi, ikiwa ni
ndani ya saa 24.
Mtu mmoja aliuawa na wengine wanne walijeruhiwa katika mtindo huo wa milipuko ya mabomu iliyofuatiwa na mashambulio ya risasi.
Polisi ilieleza kwamba watu hao wenye silaha
walivamia, kushambulia kwa mabomu umati wa watu asubuhi, kisha
kuwashambulia kwa risasi na walipokuwa wakitoroka waliwaua watu wawili
waliokuwa upande wao na kujeruhi watatu.
SOURCE: MWANANCHI
Mmoja wa washambuliaji alijeruhiwa na bomu lililolipuka wakati akikimbia, ambapo alikamatwa na kwa sasa anaisaidia polisi.
Mkuu wa Polisi wa Eneo la Wajir, Isaiah Odhiambo alisema kwa sasa wameimarisha ulinzi kwenye eneo hilo.
Wataalamu waanza kazi
Wataalamu wa mabaki ya mabomu wa Kenya na wa nchi
za kigeni wameanza kufanya upekuzi kwenye jengo la kibiashara la
Westgate, baada ya taarifa za kudhibitiwa kwa wavamizi kwa siku nne.
Upekuzi huo umeanza kufanyika huku kukiwa na
mkakati wa kimamlaka wa kuhakikisha kwamba mikakati ya taifa hilo katika
kukabiliana na ugaidi inapitiwa upya.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya alikaririwa na
BBC akisema jana kwamba wataalamu hao wameanza upekuzi huo, huku taifa
likiendelea na siku tatu za maombolezo kuanzia juzi.
Wataalamu hao wa Kenya wameanza upekuzi huo kwa
ushirikiano na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Canada na Interpol kwa
ajili ya kufuatilia vinasaba (DNA) na alama za vidole ili kubaini
wahusika wa tukio hilo.