Na Raymond Kaminyoge
Posted Alhamisi,Septemba26 2013 saa 24:0 AM
Posted Alhamisi,Septemba26 2013 saa 24:0 AM
Kwa ufupi
“ Ukiona mwenzako ananyolewa na wewe tia maji, vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe ulinzi hasa kwenye mikusanyiko ya watu,”
Dar es Salaam. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Samuel Sitta amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuacha
kufanya kazi kwa mazoea, bali viimarishe ulinzi ili kukabiliana kuweza
matukio ya kigaidi.
Sitta alisema hayo jana baada ya kufungua mkutano wa Chama cha Waajiri Tanzania (Ate) na sekta binafsi.
Alisema tukio la ugaidi lililotokea Nairobi nchini
Kenya ambalo limesababisha vifo vya watu 62 linaweza kutokea mahali
popote ikiwemo Tanzania.
“ Ukiona mwenzako ananyolewa na wewe tia maji,
vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe ulinzi hasa kwenye mikusanyiko
ya watu,” alisema.
Alisema vyombo vya ulinzi vinatakiwa kuwa macho muda wote ili kukabiliana na hatari yoyote inayoweza kutokea.
“Tunawapa pole wenzetu wa Kenya kwa maafa hayo,
nasi tuchukue tahadhari kwa sababu magaidi hawasemi ni lini watakuja
kuvamia,” alisema.
Akizungumzia tukio hilo, Sitta alisema ni la
kutisha ambalo linalaaniwa na kila mpenda amani na kwamba magaidi hao
wanatakiwa kusakwa popote walipo,ili waweze kuchukuliwa hatua za
kisheria.
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI