Arusha. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu
za Serikali,(PAC) Zitto Kabwe amesema kiasi cha Dola 2 bilioni za
Marekani, zinapotea serikalini kila mwaka kwa kutoroshwa nje ya nchi au
katika ukwepaji wa kodi .
Zitto alitoa taarifa hiyo jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha.
Zitto, alisema hata hivyo tatizo hilo, si tu kwa
Tanzania pekee yake na kwamba taarifa za kimataifa zinaeleza kuwa kwa
bara la Afrika , kiasi cha Dola 700 bilioni zanatoroshwa nje ya bara
kila mwaka.
Alisema fedha hizo ni zaidi ya misaada yote inayotolewa kwa nchi za Afrika.