Sunday, 13 October 2013

KONTENA LILILOSHEHENI MAFUVU YA BINADAMU LAKAMATWA HUKO KENYA


1
 Wengi wa waliopata taarifa hii wanashangaa imekuwaje ni viungo vya binadamu tu vimepatikana kwenye kontena vinaingizwa Kenya? Vilikuwa vinapelekwa wapi? Kazi yake nini?

Taarifa iliyoripotiwa na Citizen TV Kenya inasema shehena hii ilikamatwa baada ya kupitishwa kwenye bandari ya Mombasa.
Inasemekana kuwa imesafirishwa na mwanasiasa maarufu ambaye kabla ya kukamatwa alisema ilikuwa ni bidhaa za nyumbani ambapo ilipofikishwa kwenye kituo cha ukaguzi wa mashehena cha Changamwe na kupatikana na vikaragosi vya mafuvu na mifupa ya binadamu kisha amri ikatolewa ya kontena hilo kukamatwa.

Baadhi ya mifupa ya binadamu iliyopatikana ni pamoja na mafuvu, miguu na mikono pamoja na bidhaa za nyumbani ambapo vyote kwa pamoja vilikuwa vinasafirishwa. 
Afisa wa maswala ya uhusiano mwema wa KRA, Fatuma Yusuf alithibitisha kuwa shehena hii iliingia kutoka China siku ya pili ya Oktoba 2013 kabla ya kugundulika ilikuwa na vikaragosi vya kutisha ikiwemo mifupa ya binadamu.

Mpaka sasa uchunguzi wa shehena hiyo unaendelea lakini baadhi ya wakazi wa Mombasa wameonesha wasiwasi wao na kusema ipo haja ya serikali kutoa ripoti ya ibada ya kishetani ambayo inasemekana kubuniwa na Rais Mstaafu Daniel Arap Moi miaka kadhaa iliyopita.
12
11
13
14
 15
7
8
9
10
 5
3 
SOURCE: AZIMIO LETU