Vikosi vya jeshi la Ujerumani vimeondolewa kutoka jimbo la Afghanistan
la Kunduz muongo mmoja baada ya majeshi hayo kuwasili katika jimbo hilo.
Hatua hiyo inawakilisha hatua muhimu kuelekea kuondolewa kwa majeshi ya NATO nchini humo.
Miaka kumi baada ya Ujerumani kuanza kuweka majeshi yake katika jimbo lenye matatizo la kunduz ,jeshi la Ujerumani Bundeswehr limetangaza kuwa limefikisha mwisho ujumbe wake jana siku ya Jumamosi(19.10.2013).
"Tumekamisha kwa mafanikio operesheni ya "kujiondoa", amesema luteni kanali Heiko Diehl baada ya kuwasili katika kituo cha jeshi la Ujerumani nchini Afghanistan katika mji wa Mazar-i-Sharif.
Wajivunia mafanikio
"Tunajivunia kile wanajeshi wetu walichofanikisha katika jimbo la Kunduz hadi katika dakika ya mwisho walipokuwa hapo," amesema Vollmer.
Jeshi la Ujerumani Bundeswehr lilikabidhi rasmi kambi yao kwa jeshi la usalama la Afghanistan katika sherehe iliyofanyika hapo Oktoba 6.
Hata hivyo , operesheni za usafirishaji zilichukua muda zaidi, ambapo majeshi yaliwasili hatimaye katika mji wa Mazar-i-Sharif asubuhi ya Jumamosi.
Mlolongo wa magari 119 , ikiwa ni pamoja na magari chapa Marder ya kivita , na wanajeshi 441 wamesafiri kilometa 300 kwa siku mbili.
Kuwekwa kwa jeshi la Ujerumani katika jimbo la Kunduz kunawakilisha mara ya kwanza kwa majeshi hayo kuhusika katika mapambano tangu vita vikuu vya pili vya dunia.
Msaada bado waendelea
Kwa hatua hiyo , kituo cha Mazar-i-Sharif kinakuwa cha mwisho kwa Ujerumani nchini Afghanistan. Hata hivyo operesheni katika jimbo la Kunduz bado zinaendelea , kutokana na kuwapo wanajeshi 300 wa dharura ambao watawekwa katika eneo hilo ili kusaidia majeshi ya Afghanistan.
Operesheni ya Kunduz imedumu takriban kwa miaka kumi kamili, ambapo vikosi vya kwanza vya ujerumani viliwasili katika eneo hilo Oktoba 25, 2003. Uwekaji wa jeshi hilo katika eneo hilo la jimbo jirani la Baghlan umethibitisha kuwa miongoni mwa maeneo ya hatari sana kwa majeshi ya Ujerumani, ambapo wanajeshi wengi waliuwawa kuliko kokote kwingineko.
Baada ya marekani na Uingereza, Ujerumani ndio ilikuwa inachangia wanajeshi wengi zaidi katika jeshi hilo la kimataifa linalosaidia kuweka usalama nchini humo.
Majeshi ya kimataifa yanatarajiwa kufikisha mwisho operesheni za mapambano mwishoni mwa mwaka 2014, na kusafisha njia baadaye kwa ujumbe wa msaada wa mafunzo kulisaidia jeshi la Afghanistan.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rc/mkg(AFP,DPA) DW-English web
Mhariri:Caro Robi
SOURCE: DW
Miaka kumi baada ya Ujerumani kuanza kuweka majeshi yake katika jimbo lenye matatizo la kunduz ,jeshi la Ujerumani Bundeswehr limetangaza kuwa limefikisha mwisho ujumbe wake jana siku ya Jumamosi(19.10.2013).
"Tumekamisha kwa mafanikio operesheni ya "kujiondoa", amesema luteni kanali Heiko Diehl baada ya kuwasili katika kituo cha jeshi la Ujerumani nchini Afghanistan katika mji wa Mazar-i-Sharif.
Mlolongo wa magari ya jeshi la Ujerumani ukiondoka Kunduz
Kukamilika kwa hatua ya Ujerumani kuviondoa vikosi vyake pia kumesifiwa
na kamanda wa eneo hilo wa jeshi la kimataifa linaloongozwa na NATO
linalotoa msaada wa usalama kaskazini mwa Afghanistan, meja jenerali
Jörg Vollmer.Wajivunia mafanikio
"Tunajivunia kile wanajeshi wetu walichofanikisha katika jimbo la Kunduz hadi katika dakika ya mwisho walipokuwa hapo," amesema Vollmer.
Jeshi la Ujerumani Bundeswehr lilikabidhi rasmi kambi yao kwa jeshi la usalama la Afghanistan katika sherehe iliyofanyika hapo Oktoba 6.
Hata hivyo , operesheni za usafirishaji zilichukua muda zaidi, ambapo majeshi yaliwasili hatimaye katika mji wa Mazar-i-Sharif asubuhi ya Jumamosi.
Mlolongo wa magari 119 , ikiwa ni pamoja na magari chapa Marder ya kivita , na wanajeshi 441 wamesafiri kilometa 300 kwa siku mbili.
Kuwekwa kwa jeshi la Ujerumani katika jimbo la Kunduz kunawakilisha mara ya kwanza kwa majeshi hayo kuhusika katika mapambano tangu vita vikuu vya pili vya dunia.
Wanajeshi wa Ujerumani wakiwa na polisi wa Afghanistan
Sherehe hapo kabla mwezi huu zilihudhuriwa na waziri wa mambo ya kigeni
Guido Westerwelle na waziri wa ulinzi Thomas de Maiziere, ambaye alisema
katika hotuba kuwa Kunduz ilikuwa "sehemu muhimu sio tu kwa jeshi la
Ujerumani Bundeswehr, lakini pia jina Kunduz linabaki kuwa alama ya
mashambulizi ya anga yaliyoamrishwa katika eneo hilo ambayo
yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 100 na kuwajeruhi wengine 11
Septemba mwaka 2009, wengi wao wakiwa ni raia.Msaada bado waendelea
Kwa hatua hiyo , kituo cha Mazar-i-Sharif kinakuwa cha mwisho kwa Ujerumani nchini Afghanistan. Hata hivyo operesheni katika jimbo la Kunduz bado zinaendelea , kutokana na kuwapo wanajeshi 300 wa dharura ambao watawekwa katika eneo hilo ili kusaidia majeshi ya Afghanistan.
Operesheni ya Kunduz imedumu takriban kwa miaka kumi kamili, ambapo vikosi vya kwanza vya ujerumani viliwasili katika eneo hilo Oktoba 25, 2003. Uwekaji wa jeshi hilo katika eneo hilo la jimbo jirani la Baghlan umethibitisha kuwa miongoni mwa maeneo ya hatari sana kwa majeshi ya Ujerumani, ambapo wanajeshi wengi waliuwawa kuliko kokote kwingineko.
Waziri wa ulinzi Thomas de Maizière (kulia)na Guido Westerwelle(kushoto) wakiwa katika kambi ya Mamal
Zaidi ya wanajeshi 3,800 wanabakia nchini Afghanistan , ambapo zaidi ya
wafanyakazi 5,350 wa jeshi hilo wakiwa katika eneo hilo wakati
operesheni hizo zikiwa katika kwango chake cha juu. Zaidi ya wanajeshi
1,400 wa Ujerumani walikuwa Kunduz kwa wakati mmoja.Baada ya marekani na Uingereza, Ujerumani ndio ilikuwa inachangia wanajeshi wengi zaidi katika jeshi hilo la kimataifa linalosaidia kuweka usalama nchini humo.